Judith Ferdinand,Timesmajira
Online,MwanzaHalmashauri ya Manispaa ya Ilemela imefanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni 7,za mapato ya ndani hadi kufikia Desemba 31,2024, ikiwa sawa na asilimia 47,ya lengo la mwaka wa fedha wa 2024/2025,ambapo imekusudia kukusanya zaidi ya bilioni 14.9.
Akisoma taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,Januari 31,2025 katika kikao cha Baraza la Madiwani wa cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/25(Oktoba-Desemba),Kaimu Mkurugenzi wa Halmsahauri hiyo,Egidy Teulas,amesema kiasi hicho ni sawa na asilimi 93.8,ya lengo la nusu mwaka.
Teulas,amesema katika robo ya pili ya mwaka huu wa fedha zaidi ya milioni 270.9,za mapato ya ndani ,zilielekezwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo na kati ya fedha hizo,milioni 70 kwa ajili ya ununuzi wa eneo ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Nyasaka.
Milioni 25,kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Magaka,zaidi ya milioni 23.9,kwa ajili ya ununuzi wa viti na meza 350 kwa shule za sekondari,milioni 23.0, kwa ajili ya ununuzi wa madawati 325 kwa shule za msingi awamu ya kwanza na milioni 18 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo shule ya sekondari Bujingwa.
Pia amesema,pamoja na miradi hiyo ,Halmashauri imeendelea kutekeleza miradi mingine ya maendeleo kwa fedha za mapato ya ndani yenye thamani ya zaidi ya bilioni 2.4,ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba katika hospitali ya Wilaya ya Ilemela milioni 300 huku ukamilishaji wa hospitali hiyo ya Wilaya milioni 239.
Ujenzi wa bweni shule ya sekondari Wavulana ya Bwiru milioni 130,ukamilishaji wa bwalo shule ya sekondari Sangabuye zaidi ya milioni 113.3,ununuzi wa vifaa tiba zahanati milioni 100 na utekelezaji wa miradi kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo zaidi ya milioni 83.7.
“Halmashauri imeendelea kutekeleza miradi mingine ya maendeleo kwa fedha kutoka Serikali Kuu yenye thamani ya zaidi ya bilioni 2.5,ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji,”amesema.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga,amesema kazi ya ukusanyaji mapato ni la ushirikiano hivyo amewaomba Madiwani kuendelea kushirikiana na watendaji katika suala hilo.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Ilemela,Mariam Msengi,amewataka Madiwani hao kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao pamoja na ukusanyaji wa mapato.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo akiwemo Diwani wa Kata ya Pasiansi, Rosemary Mayunga, amesema,taarifa hiyo ni nzuri na imesheni kila upande lakini amesisitiza elimu awali ipewe kipaumbele zaidi kwani ndio msingi wa elimu.
Naye Diwani wa Kata ya Shibula,Dede Swila,amesema taarifa hiyo imesheheni miradi ya maendeleo hususani katika Kata yake miradi inaendelea ikiwemo elimu msingi na sekondari.
More Stories
Manispaa ya Shinyanga yaandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza kwa 99%
TAKUKURU yabaini miradi nane yenye dosari
Madiwani Ilemela wapitisha rasimu ya bajeti bilioni 84.3