
Na Israel Mwaisaka, Rukwa
Katibu tawala wa Wilaya Sumbawanga mkoani Rukwa Wakili Gabriel Masinga amewataka mafundi kujiunga na mfumo wa Nest utakaowawezesha kuomba kazi mbalimbali zinazotolewa na Serikali itakayowasaidia kujikwamua zaidi kiuchumi.
Wito huo ameutoa jana mjini Sumbawanga alipokuwa akifungua mkutano wa mafundi ambapo aliwataka wachangamkie fursa zinazotolewa na Serikali kwa kuhakikisha wanajiunga na mfumo huo ambao umetoa fursa kubwa kwa mafundi bila ya kujali uzoefu wao na Kwenda kufanya kazi zinazotolewa na Serikali.
Pia aliwataka mafundi hao kwa umoja wao kukutana na taasisi za kifedha na kupata mikopo ikiwemo Ile inayotolewa na serikali bila ya riba na kuwa ili waweze kuendelea kiuchumi ni lazima wakope ili wapate mitaji ya kuendeshea shughuli zao za kiufundi.
Wakili Masinga alifafanua wapo mafundi vijana wanaoweza kunufaika na programme mbalimbali za uwezeshaji vijana kiuchumi kupitia Serikali na kupitia umoja huo wa mafundi watakua na nafasi kubwa ya kunufaika na Fursa hizo.
Na aliwataka mafundi kuachana na ubinafsi badala yake washirikishane katika kazi mbalimbali wanazozipata kwa kupeana kazi na kulipana ujira na kuwa kwa kufanya hivyo kutawawezesha kukamilisha kazi kwa wakati na tija kitu kitakachowajengea uaminifu kwa waajiri wao na kujijengea heshima.
Sambamba na hilo aliwataka mafundi kupitia umoja wao kujenga utamaduni wa kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo kufanya usafi katika taasisi mbalimbali za Umma na Kutoa damu ambayo itawasaidia Watu wenye uhitaji na kuweza kuokoa maisha ya watu.
Alidai kuwa kitendo cha mafundi kujitokeza kwenye shughuli za kijamii kama walivyojitokeza kufanya usafi maeneo mbalimbali ya kijamii mjini Sumbawanga kunawajengea mazingira ya kuaminika na jamii kuwaona kwamba na wao ni sehemu ya jamii.
Alisema kwamba kwa sasa wanaweza Kwenda mbali zaidi hata Kwenda kuwaona Mayatima,Wajane na wengine wenye uhitaji kwa kushirikiana katika mambo mbalimbali na kuona kwamba na wao ni sehemu Yao.
Mkutano huo wa mafundi ulipata nafasi ya kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu mafundi ikiwa ni pamoja na kujaza baadhi ya nafasi za uongozi zilizokuwa waziri kutokana na sababu mbalimbali

More Stories
Msigwa atoa wito kuandikwa habari za vijijini
Exim Tanzania yaunga mkono uhifadhi wa Mazingira,Maendeleo
TCB kugawa pembejeo kidijitali