Na Esther Macha, Timesmajira Online,Rungwe
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya,limesema licha ya uzalishaji wa maziwa kuwa mkubwa, mapato yake yamekuwa kidogo,hivyo limetaka Halmashauri kushughulikia changamoto hiyo kwa kudhibiti wizi wa maziwa ambao unasababisha upotevu wa mapato.
Hayo yamesemwa January 27,2025 ,kwenye mkutano maalum wa Baraza la Madiwani ambao ulikuwa ukijadili rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Akichangia hoja ya rasimu ya bajeti katika mkutano huo wa Baraza la Madiwani,Diwani wa Kata ya Malindo,Nicodem Mwakalile amesema kuwa ukusanyaji wa maziwa umekua mkubwa lakini mapato yake ni madogo .
“Kwenye Kata yangu kwa mwaka nakusanya lita mil.17 za maziwa,ajaribu kuangalia kama Halmashauri nzima inafikiria kukusanya lita mil.60,watalaam wetu watusaidie nafikiri kuna changamoto ambayo hatuioni kwa muda mrefu ambayo imekuwa sumbufu hasa hawa wakusanyaji binafsi.Kwenye kituo changu maziwa yamepungua kutoka lita 5000 ,ambayo ilikuwa inakusanywa kwa siku mpaka kufikia lita 3000,”amesema Diwani huyo.
Elizabeth Ngaga ni Diwani viti maalum Wilaya ya Rungwe,amemuomba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuwa nusu ya miradi iliyobaki ikatekelezwe kwenye Kata zao.
Mkuu wa Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Adam Nkhangaa,amesema mpaka sasa wamekamata magari matatu yalioenda kinyume na taratibu za ubebaji maziwa na kuyapiga faini.
“Madiwani niwaombe muwe wavumilivu kwani tayari utekelezaji wake umeanza ili kuendelea kuweka msingi thabiti wa ukusanyaji mapato ya halmashauri yetu,lakini ukipita kuanzia saa tisa usiku kuna wanawake wafanyabiashara,pembezoni mwa barabara ambao wanauza maziwa na wengi wao hawaendi kwenye maeneo husika kuchukua maziwa,”.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Renatus Mchau,amesema kutokana na changamoto hiyo watawasiliana na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD),kuweka geti lingine huku wakitegemea kubadilisha na kupeleka mbele kituo cha kukusanyia mapato lengo ni kudhibiti.
More Stories
TARURA Kilindi kutumia bil.5.2 bajeti 2025/26
Madiwani Kilindi wapitisha bil.36.8 bajeti 2025/26
THBUB yatoa tamko kulaani mauaji ya Jumanne Juma