Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki amemkabidhi rasmi Dkt. Robert Fyumagwa majukumu ya kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania- TAWIRI.
Dkt. Robert Fyumagwa anatekeleza majukumu ya Taasisi hiyo kufuatia aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori-TAWIRI, Dkt.Simon Mduma kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Kupitia hatua hiyo tayari Dkt.Fyumagwa ameanza rasmi kutekeleza majukumu ya Taasisi hiyo kuanzia tarehe 17 Agosti, 2020.
Akizungumza Jijini Arusha katika Kikao na Menejimenti ya TAWIRI, Dkt. Nzuki amewataka watumishi hao kumpa ushirikiano Dkt. Fyumagwa katika kutekeleza majukumu yake ikiwa pamoja na kuimarisha shughuli za utafiti wa Wanyamapori pamoja na kuendeleza sekta ya wanyamapori nchini.
More Stories
Puma Energy Yazindua Mradi wa Umeme wa Jua kwa Kiwanda cha Alliance One
Mkuu wa JKT awatoa hofu wazazi asema,JKT ni mahali salama
‎Serikali Yatilia Mkazo Utekelezaji wa Upandishaji Vyeo kwa Watumishi wa Umma