Na Joyce Kasiki,Timesmajira online Dodoma
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewaasa wananchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu kutokuwa kishawishi cha wagombea kutoa rushwa .
Aidha imewataka wananchi kutowachagua wagombea wanaotaka nafasi za Uongozi kwa kutoa rushwa .
Akizungumza kwenye maonesho ya wiki ya Sheria nchini yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere jijini Dodoma,Mchunguzi Kutoka ofisi ya TAKUKURU Idda Siriwa amesema wakati mwingine wananchi nao wanakuwa katika mitazamo ya kutaka rushwa kwa wagombea.
“Kwa hiyo Ili kuwapa wananchi uelewa juu ya masuala ya rushwa ,huwa tunatoa Elimu kwa wananchi, kwani nao wapo katika mitazamo ya kushawishi wagombea kutoa rushwa,tunawaombea wananchi
wasiwe kishawishi cha mgombea kutoa rushwa,
“Maana leo akikosea akachagua kiongozi mtoa rushwa ajue ana mateso kwa kipindi Cha miaka mitano ijayo..,tunaamini kiongozi akiingia madarakani kwa rushwa hawezi kuwa na utendaji mzuri katika kuleta maendeleo ya wananchi na katika Uongozi kwa ujumla ,maana tunaamini kiongozi yeyote anayetoa rushwa na yeye ni mpokea rushwa.”amesema Idda
Kufuatia Hali hiyo amesema,TAKUKURU imejipanga kutoa Elimu dhidi ya wajibu wa wananchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu ambapo wanapita mtaa kwa mtaa, kata kwa kata kutoa Elimu kwa wananchi Ili wasikubali kirubuniwa maana kura yao ina thamani na wanapaswa watambue hivyo.
“Kwa hiyo tumewajenga na tunaendelea kuwajenga wananchi kwamba kipindi hiki wanatakiwa wajitambue na wathamini kura yao.”amesisitiza Siriwa
Siriwa ametaja baadhi ya madhara ya rushwa kuwa ni pamoja na kudhoofisha demokrasia,kuchaguliwa viongozi wasiofaa,huzorotesha maendeleo,hudhoofisha haki ya kuchagua na kuchaguliwa,hudhalilisha mpiga kura kwa kumthaminisha na thamani ya hongo aliyopokea.
Kuhusu Wajibu wa mwananchi na mgombea amesema ni pamoja na kuchukia rushwa,kuelimisha wengine ubaya na madhara ya rushwa kwenye uchaguzi,kuhakikisha uchaguzi unafanyika bila vitendo vya rushwa,kujiepusha na vitendo vya rushwa katika uchaguzi ,kutoa taarifa za wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na kutoa ushahidi mahakamani shisi ya wanaojihusisha na vitendo vya ryshwa
Naye Mchunguzi wa Taasisi hiyo Gabriella Gabriel amesema wanashiriki maonesho hayo katika kutekeleza jukumu lao la kuzuia na kupambana na rushwa kwa kutoa Elimu juu ya athari ya vitendo vya rushwa kwa wananchi wanaopita kwenye banda lao.
Vile vile amesema Elimu hiyo wamekuwa wakiitoa kwa njia mbalimbali ikiwemo vipindi vya radio,semina,makongamano na maonesho ya kitaifa na kinataifa ambayo wamekuwa wakishiriki.
Aidha amesema katika maonesho hayo ya wiki ya Sheria ,mbali na kutoa Elimu pia wanapokea malalamiko mbalimbali ya vitendo vya rushwa na kuvitolea ufafanuzi.
“Pia tunashiriki maonesho haya kwa sababu sisi ni Wadau wa mnyoroto na haki jinai kwani tuna mamlaka ya kuchunguza na kupeleka jalada kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kisha mahakamani Ili kuthibitisha kama mtu ana makosa ya rushwa ya kujibu au vinginevyo.amesema Gabriel
Aidha amesema,wananchi wamekuwa na muamko kutokana na Elimu wanayoipata na matokeo ni chanya kwani TAKUKURU imekuwa ikipokea taarifa mbalimbali za rushwa na kuzifanyia uchunguzi na kupeleka hadi ngazi ya Mahakama.
More Stories
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoa ushauri wa kisheria bure
CPA.Makalla atembelea miradi ya kimkakati kusini Pemba
Wanafunzi 170 wapata ufadhili wa masomo