March 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampeni Ubungo usiku kama mchana yazinduliwa

Na Mwandishi wetu Timesmajira online

HALMSHAURI ya Manispaa ya Ubungo imezindua rasmi kampeni ya Ubungo usiku kama mchana yenye lengo la  kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji na Biashara kwa masaa 24 katika siku saba za wiki .

Akizindua kampeni hiyo Jijini Dar es salaam mapema  Januari 24 , 2025, Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hassan Bomboka kabla ya kuteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai , amesema  kampeni hiyo itakuza uchumi  na  kuongeza pato kwa wafanyabiashara wakubwa,wakati na wadogo.

Amesema kampeni hiyo itafanyika kwa maarifa, umakini na utu kwani imelenga kukuza uchumi na kuongeza mapato.

“Halmshauri ya Ubungo tunazindua rasmi ajenda hii kwa sababu ya wilaya ya ubungo imekuwa ni eneo la kimkakati ambalo ndio lango la Jiji, na limekuwa likifanya kazi kubwa katika eneo la biashara katika Mkoa wa Dar es salaam”amesema Bomboka

Amesema kampeni hiyo kwa awali itaanza katika maeneo saba ya kimkakati  yaliopo katika Halmshauri hiyo ambayo ni pamoja na soko la mahakama ya ndizi, stedi kuu ya mabasi yaendao mkoani , stedi ya daladala mbezi mwisho, soko la shekilango, Manzese Baharesa, maeneo yote ya sinza, Mlimani city,  na ubungo.

Aliongeza kuwa Halmshauri hiyo itahakikisha huduma zote muhimu zinaendelea kutolewa kwa masaa 24 ikiwemo huduma za afya,huduma za kijamii, maji,umeme.

“Kupitia kampeni hii  kuhakikisha barabara, taa za barabarani zinawaka ikiwa ni tafsiri ya shughuli zinazofanyika usiku zinakuwaje mchana”amesema.

Aidha amesema kuwa mpaka sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 80 huku asilimia 20 iliyobakia ikijikita katika  kuimarisha miundombinu.