Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo amechangia Shilingi milioni tatu katika mfuko wa vijana maofisa usafirishaji maarufu Bodaboda katika kituo cha Sabasaba A mkoani Dodoma.
Bodaboda hao wanaofahamika pia kwa jina la kituo chao VIJANA NA SAMIA leo walipata ugeni huo rasmi ambao walizindua shina la Wakereketwa la UVCCM la Vijana wa Samia soko la Sabasaba na kibanda kwa ajili ya kupumzikia wakati wa jua na mvua ambacho kimejengwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde.
Katika Unduzi huo Jokate aliongozana na vijana zaidi ya 500 ambao wamekuwa wakisaidia maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa utakaofanyika Januari 18 hadi 19 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.
Jokate amewataka vijana hao kuendelea kuamini serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani imekuwa ikithamini vijana katika kila sekta kuhakikisha wanapiga hatua katika shughuli za uzalishaji.
Kwa upande wa Mavunde ameahidi kuwafungia televisheni na king’amuzi katika tawi hilo ili kuwawezesha kufuatilia taarifa mbalimbali zinazotokea ndani na nje ya Nchi.
More Stories
Wazazi wa Wanafunzi Sekondari ya Muhoji waamua kutoa chakula kwa watoto wao
Wizara ya Nishati yawasilisha utekelezaji wa bajeti 2024/2025 kwa Kamati ya kudumu ya bunge Nishati na Madini
Watanzania milioni 13.5 kusambaziwa umeme ifikapo 2030 kutoka milioni 5.2 ya sasa