BARCELONA, Hispania
RAIS wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu amethibitisha kuwa kocha wa timu hiyo Quique Setien, wapo mbioni kumfungashia virago kwa kile kinachodaiwa timu kufanya vibaya msimu huu katika Ligi Kuu Hispania La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Licha ya kocha Setien kuwa katika msimu mgumu kwa kushindwa kunyakuwa ubingwa lakini Bartomeu alisema hadharani kuwa kocha huyo atapewa msimu mwingine.
Hata hivyo, baada ya klabu hiyo kukubali kichapo cha paka mwizi cha kufungwa magoli 8-2 dhidi ya Bayern Munich katika michuano ya Ligi ya Mabingwa UIaya hatua ya robo fainali klabu hiyo imeamua kumpiga chini Setien.
Kuondoka kwa kocha huyo, mrithi wake huwenda akawa Muholanzi Ronald Koeman, Mauricio Pochettino, Xavi na Massimiliano Allegri mmoja kati yao.
Mbali na kocha Setien pia nohadha wa Barcelona Lionel Messi amedhamiria kuondoka klabuni kwa kile anachodao kutafuta changamoto zingine kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025