Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameongoza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, kutembelea Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo jijini Dodoma, ili kukagua maendeleo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika Januari 18 na 19, 2025.
Ukumbi huo, wenye uwezo wa kuchukua takriban watu 3,000, unakarabatiwa kwa kiwango cha juu, ili kuhakikisha mazingira bora kwa mkutano huo muhimu, ambao utakuwa na agenda kadhaa, ikiwemo kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), kufuatia kujiuzulu kwa Abdulrahman Kinana mwaka jana.
Balozi Nchimbi, akiwa ameambatana na Manaibu Katibu Mkuu wa CCM, John Mongella (Bara) na Dkt. Mohamed Said Dimwa (Zanzibar), pamoja na wajumbe wa Sekretarieti, alishuhudia kasi kubwa ya maandalizi hayo, huku akiwapongeza wahusika kwa jitihada zinazofanywa kuhakikisha kila kitu kinakuwa tayari kwa wakati.
Kwa mujibu wa Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla, amesema, maandalizi ya mkutano huo yamefikia hatua nzuri, ambapo alitangaza rasmi hivi karibuni huku akibainisha kuwa mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango