January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanzania,Uturuki kushirikiana kuinua sekta ya utalii nchini

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online

BOD,I ya Utalii Tanzania (TTB) imeanzisha ushirikiano wa kimkakati na shirika la ndege la Uturuki (Turkish airlines),kwa mkataba wa miaka mitatu ukilenga kukuza utalii wa Tanzania katika masoko ya kimataifa.

Ushirikiano huo unalenga kutumia mtandao wa shirika hilo unaojumuisha zaidi ya ndege 490 zinazohudumia miji 411 duniani kote zikiwemo 61 barani Afrika.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa (TTB) Ephraim Mafuru, amesema mpango huo unalenga kuongeza idadi ya watalii na wawekezaji nchini,ambapo Turkish airlines itaonesha vivutio vya Tanzania kwenye ndege, tovuti na ofisi zao huku ikitoa punguzo la nauli kwa safari za utalii.

“Huu ni mwanzo wa mikakati yetu ya kushirikiana na mashirika ya ndege, tunatarajia kuvutia watalii zaidi na wawekezaji pamoja na kukuza sekta ya utalii na uchumi wa taifa,” amesema Mafuru.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtyendaji wa Turkish airlines Abdulkadir Karaman,ameeleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kufanikisha lengo la kufanya Tanzania inakuwa kivutio cha utalii duniani.

“Kauli mbiu yetu ni panua ulimwengu wako na tunarekodi ya Guinness kwa kusafiri hadi nchi zaidi duniani, ambapo hii inathibitisha uwezo wetu wa kuunganisha watalii kila kona ya dunia hadi Tanzania,” amesema Karaman.