January 7, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Mwinyi atenga Bil. 300/- kila mwezi kulipa madeni

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

RAISI wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia Wananchi kuwa Serikali inatenga kiasi cha takriban shillingi Billioni 300 kwa mwezi kwa ajili ya kulipa Madeni ya Nchi.

Rais Dk, Mwinyi ameeleza kuwa wakati Serikali inakopa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo Ina Akaunti Maalum inayoweka Fedha za kutosha Kulipa Madeni hayo ambayo sasa ina kiasi cha Shillingi Biliioni Mia Sita.

Rais Dk,Mwinyi ametoa Tamko hilo alipofungua Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini,Mkoa wa Mjini Magharibi
kilichojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF).

Amefahamisha kuwa deni ililonalo Zanzibar kwa sasa ni Shillingi Trilion 1.2 linalohimilika na kuwa na Uwezo kukopesheka tena kutokana na utaratibu huo uliopo Serikali inaweza kulilipa ndani kipindi cha miaka miwili.

Aidha ameeleza kuwa Wakati Serikali ya Awamu ya Nane inaingia Madarakani deni la Serikali lilikuwa Shillingi Bilioni Mia nane na sasa baada ya miaka minne limepanda hadi kufikia Trilioni 1.2

Rais Dk, Mwinyi amekanusha vikali taarifa zilizotolewa na Wapinzani hivi karibuni kuwa Zanzibar ina deni linalofikia Trilioni 2.8 sawa na ongezeko la asilimia 208 kuwa za Uongo na Propaganda za Kisiasa zisizo sahihi.

Amesisitiza kuwa Serikali inakopa kwa nia njema ya Kuendesha Miradi ya Maendeleo yenye tija na maslahi kwa nchi na sio Vyenginevyo.

Akizungumzia suala la Uwekezaji Rais Dk, Mwinyi amekemea Vikali Suala la Urasimu ndani ya Taasis za Serkali unaokumbana nazoTaasisi zinazotaka kuwekeza nchini.

Akiwekea Msisitizo suala hilo Dk,Mwinyi amezitaka taasisi kutoa taarifa kwake pale zinapokabiliana na Urasimu.

Akizungumzia kituo hicho jipya cha Mabasi ameutaka Mfuko wa Hifadh ya Jamii ZSSF kuwa na Mpango maalum wa Matunzo na Usafi na kuandaa ajira Maalum kwa Vijana kwa ajili kutoa huduma za usafi.

Rais Dk, Mwinyi amefahamisha kuwa Serikali inakuja na Mpango Mkuu wa Usafiri utakaoifanya nchi kuwa na Usafiri wa Kisasa na Huduma Bora.

Mpango huo utajumuisha Ujenzi wa Vituo vya Kisasa vya Mabasi katika Maeneo ya Chuini,Jumbi ,Mwera na Mwanakwerekwe pamoja na Kijangwani ,Malindi na Mnazi Mmoja kwa Eneo la Mjini kusisitiza kuwa kabla Mwisho wa Mwaka huu Zanzibar itaanza kutumia Mabasi Ya Umeme.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Fedha na Mipango Dk,Sada Mkuya Salum amefahamisha kuwa Uwekezaji unaofanywa katika Miradi mbalimbali nchini Unaongeza thamani ya Nchi kiuchumi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dk,Juma Malik Akil amefahamisha kuwa Uchumi wa Zanzibar Unategemea sekta ya huduma hususan Utalii na Usafiri kwa asilimia 50 na kuchangia ukuaji wa sekta nyengine za kiuchumi .

Amebainisha kuwa mifumo ya Kisasa ya Usafiri inalenga kuviunganisha Vijiji vyote vya Zanzibar na Usafiri wa Kisasa.

Naye Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Nassor Shaaban ameeleza kuwa zaidi ya Shillingi Bilioni 700 zimeingizwa sokoni na Mfuko huo kwa lengo la kuimarisha Uchumi na kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 250 zimelipwa kwa wastaafu ndani ya miaka minne ya awamu ya nane na wastaafu 15,000 wanaendelea kulipwa pensheni kwa mafanikio kila mwezi.