Na Hadija Bagasha, Timesmajira Online,Tanga
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa Tanga imejivunia kukusanya kiasi cha bilioni 153.6,kwa kipindi cha Julai hadi Novemba,2024 tofauti na kiwango cha bilioni 78 walichokusanya mwaka jana ndani ya kipindi hicho.
Akizungumza Desemba 23,2024 wakati wa ziara yao kutembelea wafanyabiashara mbalimbali jijini Tanga Meneja wa TRA Mkoa Tanga Thomas Masese, amesema mwaka 2024 umeanza kwa mafanikio katika ukusanyaji wa mapato ambapo kuanzia Julai hadi Novemba,lengo lilikuwa kukusanya bilioni 131.6 lakini wamekusanya bilioni 153.6 sawa na ufanisi wa asilimia 117.
Wateja waliotembelewa na Mamlaka hiyo wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano ,na kuongeza kasi ya ulipaji kodi kwa maendeleo ya nchi huku wakilaani baadhi ya wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi.
Mamlaka hiyo imeitaka jamii kujenga utamaduni wa kudai risiti mara wanapofanya biashara,ikiamini kama jamii itaimarisha utamaduni wa aina hiyo ,ongezeko la makusanyo yanaweza kuongezeka mara dufu hapo mwakani.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba