December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa Kwanza wa Rais ziarani Pemba

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Othman Masoud Othman, jioni ya leo Disemba 23, 2024, amewasili Kisiwani Pemba kwaajili ya Ziara Maalum, inayojumuisha Shughuli za Serikali, Chama na jamii.

Katika Uwanja wa Ndege wa Pemba, Mheshimiwa Othman amepokelewa na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Chama, na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Ndugu Rashid Hadid, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Bi. Mgeni Khatib Yahya.