Na Hadija Bagasha, Timesmajira Online,Tanga
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania Kanda ya Kaskazini (TFS),imewataka watu waliovamia misitu ya hifadhi, kuondoka mara moja kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria dhidi yao.
Wito huo umetolewa Desemba 19,2024,na Kamanda wa Uhifadhi wa TFS,Kanda ya Kaskazini James Nshare,wakati akizungumza katika kikao na wadau wa uhifadhi kuelezea hali ya uhifadhi wa misitu kwenye Kanda hiyo.
Amesema katika kuhakikisha wanalipa kipaumbele suala hilo,wamejipanga kutumia teknolojia za kisasa na watatumia ndege nyuki (Drones) zitazo wasaidia kuangalia maeneo ya wavamizi na kuchukua hatua stahiki mapema.
Pia amesema,kwa maana misitu mingine ni mikubwa na huko ndani kuna watu wanafanya kilimo cha madawa ya kulevya, kwa sababu ni ndani sana na watumishi ni wachache hivyo watatumia teknolojia za kisasa ili kuweza kuwaondoa .
“Serikali itachukua hatua muda wowote kuanzia sasa, hatutaweza kuvumilia muendelee kuteketeza misitu kwa maslahi yenu binafasi, sio Tanga na maeneo yote Kanda hii ,tutashirikiana na vyombo vyengine kuhakikisha tunawaondoa,”amesema.
Kamanda huyo wa Kanda alisema pia kitu kingine ambacho kinachangia ni kilimo cha kuhama hama kwa maana wanapohama wanafyeka maeneo makubwa na kufungua maeneo mapya na kufanya hivyo wanaathiri uoto wa asili.
Awali akizungumza wakati akifunga kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Korogwe William Mwakilema,amesema Serikali inaendelea na mpango wake wa kuondoa wananchi waliovamia msitu wa Bondo,Wilaya ya Kilindi na kufanya uharibifu kutokana na shughuli za kibinadamu wanazozifanya ikiwemo kilimo,ukataji miti kwa ajili ya mkaa.
More Stories
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais
NIDA yawakumbusha wananchi kuchukua vitambulisho vyao