Na Penina Malundo,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA),imesema mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa unaonesha kuwa katika kipindi cha saa 6 zilizopita,Kimbunga“CHIDO”kimeingia nchi kavu katika eneo la kaskazini mwa Msumbiji na kimeanza kupoteza nguvu yake huku kikielekea kusini magharibi mbali zaidi ya nchi yetu.
Taarifa iliyotolewa jana na Mamlaka hiyo imesema kutokana na ukaribu wa njia yake na maeneo ya hapa nchini, wakati Kimbunga ”CHIDO” kikiingia nchi kavu huko kaskazini mwa Msumbiji mnamo asubuhi ya jana Disemba 15,2024 kimeweza kusababisha vipindi vya mvua kwa mkoa wa Mtwara na maeneo jirani.
Imesema kwa sasa hakuna tena tishio la kimbunga “CHIDO” katika nchi yetu na hakuna madhara zaidi ya moja kwa moja yanayotarajiwa yakihusishwa na kimbunga hicho.
“Hata hivyo ikumbukwe kuwa, kwakuwa tupo ndani ya msimu wa mvua katika maeneo mengi hapa nchini, matukio ya mvua za kawaida za msimu yanatarajiwa kuendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini,”amesema.
Wametoa ushauri wa watumiaji wa taarifa za hali ya hewa na wananchi kwa ujumla kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta.
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya