January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

LGTI yaunga mkono juhudi za Dkt.Samia matumizi nishati safi nchini

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

CHUO Cha Serikali za Mitaa(LGTI)-Hombolo kimesema ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi wamejadili namna nzuri ya kutoa elimu kwa  wananchi juu ya matumizi ya nishati hiyo kwa maendeleo ya nchi.

Hayo yamesemwa,Jijini hapa leo,Disemba 4,2024 na Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma,Tafiti na Ushauri kutoka LGTI, Professa Magreth Bushesha wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la 16 lilifanyika Chuo hapo ambalo lilifunguliwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Adolf Ndunguru lililokuwa limebeba mada ya kuanza kutumia nishati safi kwa maendeleo ya ndani, changamoto na matarajio ya siku zijazo.

Ambapo kongamano hilo limewakutanisha wanazuoni ambao wamesoma chuo hicho na wale ambao wanaendelea kusoma katika kwa pamoja wamechakata mawazo mbalimbali kwajili yakuleta maendeleo ya nchi kwa kutumia njia ya uelimishaji.

“Hivyo mwaka huu tumekuja na mada ya nishati safi ni kwasababu sisi kama chuo cha elimu ya juu tunawajibu mkubwa sana katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi,madhara yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi .

“Lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa analipa jambo hili kipaumbele sana,nadhani wote mnafahamu yeye dira yake inatutaka tuachane na matumizi ya nishati inayosababisha uchafuzi wa mazingira na kuleta mabadiliko ya tabia nchi.

“Hivyo sisi tukaona tunapaswa kulipa kipaumbele jambo hili tulilete sasa kwa wanazuoni wajadili,wachakate na waelimishane ili baada ya hapa tuweze kuona sisi kama chuo au wasomi walotoka kwenye chuo hiki wanawezaje kuchangia katika kuwafanya wananchi watumie nishati safi,”amesama Prof.Bushesha.

Kwa upande wake Dkt.Kenneth Nzowa,Mkuza Mitaala Mwandamizi kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania,Dar es Salaam amesema kuwa amekuja chuoni hapo kama mzungumza katika mada inayohusu masuala ya kuanza kutumia nishati safi na wamekuwa wakiangazia changamoto zilizopo na kuangalia uwezekano katika kuendelea kuhamasisha wananchi ili kupata uwezo wa kufanyia kazi kwa pamoja na kuwa sehemu ya maendeleo yao.

“Unajua hivi sasa hata Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza suala hili la nishati safi hasa hii nishati safi yakupikia nyumbani.

“Kwahiyo kwa mada hii na sisi tumekuwa tukiendelea kuiongelea sehemu mbalimbali na moja wapo ikiwa ni hapa ambayo imechukua ndiyo mada kubwa katika Kongamano hili ambayo tumeiongelea nishati safi .

“Kwahiyo tunazidi kutoa elimu kwa watu mbalimbali kutumia nishati safi wakiwemo wanafunzi mahali popote tunatoa elimu pia kwa walimu na kila mtu na tunaamini kwakufanya hivyo mtu atakapopata elimu atakuwa na uwezo sasa wakuamua kuchagua atumie nishati safi kwajili ya kuokoa mazingira,kwajili ya kuokoa afya yake na nishati ya uhakika vilevile atumie kwajili ya maendeleo yake binafsi ikiwemo kutumia mabomba yanayotumia nishati ya jua(Sola)kupata maji,kumwagilia mashamba,kupata mwanga wa kawaida ikiwemo kufanya shughuli nyingi zinazoweza kutumia umeme ili kuweza kuendeleza maisha yake ya kawaida,” amesema Dkt.Nzowa.

Ameeleza kuwa kuna changamoto ya umeme hasa vijijini ingawa serikali inajitahidi sana kuweza kumfikishia kila mwananchi umeme lakini kuna maeneo ambayo yako nje zaidi wako watu watatu kwenye kisiwa kimoja ambao wao kufikiwa kutokana na umbali kutoka kwenye gridi ya taifa ni ngumu lakini wakipelekewa nishati ya jua wanaweza kufanya jambo fulani.

“Lakini tunapoongelea nishati safi hatuongelei sola tu tunaongelea vitu  vingine vingi ,tunaongelea hata majiko aina ya jiko ambalo unaweza kutumia kabonidyoksaidi  isitoke kwa wingi sana .

“Utaona hivi karibuni Mhe.Rais ailiongoza kuwapa watu haya majiko ambayo tunasema kwamba ni majiko mazuri kwajili ya kupunguza kabonidyoksaidi ambayo inasababisha hali ya hewa kutokuwa nzuri au mabadiliko ya nchi,”amesema Dkt.Nzowa.

Aidha amesema kuwani kweli kuna gharama  kwenye nishati safi hasa mfano mtu anataka kununua sola paneli lazima ataona kuna gharama kubwa hasa anapoianzisha lakini baada ya kuwa na hiyo sola panel huko mbele hatakuwa analipa tena gharama.

“Lakini zile gharama za kuanzisha kweli ni kubwa lakini tunakuwa jambo moja ukiwa unataka kufanya kitu hata gharama kubwa utakifanya,”amesema

Hata hivyo Dkt.Nzowa amesema kuwa Serikali inaweza ikaangalia kwa namna gani inaweza kupunguza kodi katika vifaa vya sola japo kwa sasa mipango ipo yakupunguza katika ile nishati safi lakini waangalie na mlolongo wake katika kupunguza gharama hizo za kodi.