Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Pugu, Juma Orenda, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa na hatua thabiti zinazochukuliwa katika kuboresha sekta ya elimu nchini huku akisisitiza kuwa zimeleta mabadiliko makubwa, ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya shule, kuongeza upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, pamoja na kuweka mazingira bora kwa walimu na wanafunzi.
Ameeleza kuwa sera na mipango ya serikali katika sekta ya elimu zimekuwa chachu ya kuinua viwango vya elimu na kuhakikisha kuwa watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora itakayowaandaa kuwa raia wenye tija kwa taifa.
Hayo yamejiri wakati akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya misaada kwa shule za mahitaji maalum iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
“juhudi hizo zinajumuisha Uboreshaji wa miundombinu ya shule ili kuhakikisha mazingira bora ya kujifunzia.Kuimarisha elimu jumuishi, ikiwemo kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum.Mazingira wezeshi kwa walimu na wanafunzi, yanayowezesha utendaji mzuri wa kazi na maendeleo ya kitaaluma na Ushirikishwaji wa TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji, jambo linalosaidia wanafunzi kuwa tayari kwa mabadiliko ya ulimwengu wa kidigitali.” Alisema
Orenda alisisitiza umuhimu wa elimu katika kuleta maendeleo endelevu ambapo alibainisha kuwa elimu ni msingi wa kujenga jamii yenye uelewa, ustawi, na uwezo wa kukabiliana na changamoto za kiuchumi, kijamii, na kimazingira kwa njia endelevu.
Aidha, Bw. Orenda alimshukuru Mkuu wa kikundi cha wanadiplomasia wa Afrika na Balozi was Muungano wa Comoro katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, H.E. EI Badaoui Mohamed kwa ukarimu wake katika kutoa misaada, ambayo itasaidia kuboresha elimu kwa wanafunzi wa mahitaji maalum.
Katika kuhitimisha, Bw. Orenda aliahidi kushirikiana kwa karibu na serikali na washirika wa maendeleo, akisema kuwa dhamira yake ni kufanya kazi kwa bidii ili kufanikisha malengo ya kitaifa na kimataifa ya maendeleo endelevu kupitia sekta ya elimu.
Alisisitiza kuwa maendeleo ya taifa lolote hutegemea elimu imara, jumuishi, na endelevu.
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19