Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, CPA. Amos Makalla amesema chama hicho akicheki na mtu katika suala zima la kushika dola,Hivyo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu kimejipanga kuhakikisha kinashinda kwa kishindo.
CPA Makalla ameyasema hayo Novemba 23, 2024,wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam, ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka.
Amesema, kwa sasa chama hicho kinaendelea kufanya kampeni za uchaguzi huo ambazo zilizinduliwa Novemba 20 mwaka huu,katika mikoa yote nchini na ‘kujizolea’ maelfu ya wanachama kutoka vyama pinzani.
“Katika uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa tutashinda na tunataka ushindi wa kishindo, kwa jinsi ambavyo CCM tumejipanga ni sawa na kusema yajayo yanafurahisha,”amesema CPA. Makalla.
Pia amesisitiza wanachama na viongozi wa CCM kutobweteka,bali waendelee kuhamasisha wananchi kuendelea kukiamini chama hicho,na kuwataka kutokuwa warahisi baadhi ya watu kuwahada,bali wakazisake kura nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa ili wakapate ushindi wa kishindo.
“Kuna watu watakuja kuwadanganya kuwa msipende kupiga kura kwani tayari CCM imeshashinda, msikubali ni waongo waambieni sisi tunaenda kupiga kura ili kuongeza kura za kishindo,anayeombea CCM kuishusha kwa kura ya hapana huyo ni sawa na mtu anayesuburi meli uwanja wa ndege”, amesema Makalla.
Aidha amesisitiza kuwa, uchaguzi huo ni muhimu na CCM inachukulia uchaguzi huo kwa umuhimu,kwani inatambua kazi ya chama cha siasa ni kushika dola na chama hicho kinaanza na kushinda uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Kazi ya chama cha siasa kilichosajiliwa ni kuhakikisha kinashika dola na siyo kuhubiri kwenda mbinguni hayo yanafanywa na viongozi wa dini. Kwa kutambua umuhimu wa kushika dola ndio maana katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa CCM imeweka wagombea wake kwa asilimia 100 kwani hakuna Mtaa, Kijiji wala Kitongoji ambacho tumeacha, kote tumesimamisha wagombea kwa nafasi zote,amesema na kuongeza .
“Vyama vingine havina utayari na ndio maana wameshindwa kusimamisha wagombea katika nafasi zote na mpaka sasa kuna Mitaa ambayo tayari wagombea wake hawana washindani,”.
More Stories
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi