Na Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Abbass Tarimba,amesema wananchi washiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuchagua viongozi walio sahihi.Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika nchini kote Novemba 27,2024.
Tarimba,amezungumza hayo Novemba 20 mwaka huu, jijini Dar-es-Salaam, katika ufunguzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa wagombea wa CCM,ambapo amesema chama hicho ,huchagua viongozi ambao wanafukika,wenye maono na nia ya kuwasaidia wananchi, kutatua na kubeba changamoto zinazowakabili ndani ya jamii.
Aidha Mbunge huyo ameeleza kuwa Kata ya Tandale ina maeneo 6 ambayo ni Kwatumbo, Muhalitani,Sokoni,Mkunduge,Pakacha na Mtogole ambapo wamesimamisha wagombea wenye weledi wa kuwatumikia watanzania ambao ndio wapiga kura wao.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Tandale Abdallah Chief amesema, viongozi hao kutoka CCM ni lulu katika kutatua changamoto mbalimbali,hivyo amewaomba wananchi wawachague.
Naye mgombea nafasi ya Uwenyekiti wa serikali za mitaa,mtaa wa Kwatumbo Abdulbali Omari amesema kuwa akipata ridhaa ya kuchaguliwa kushika kiti hicho atahakikisha,anashughulikia suala la ulinzi na usalama kwa mujibu wa muogozo wa Serikali na wananchi wa eneo la Kwatumbo.
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo