Na George Mwigulu,Timesmajiraonline, Katavi.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpinduzi (CCM),Zanzibar,Mohammed Dimwa ameeleza kuwa chama hicho kitaendelea kuwa kiungo muhimu kati ya wananchi na serikali kwenye kuwaletea maendeleo.
Kiongozi huyo wa CCM amezungumza hayo Novemba 20, 2024 wakati akizindua kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 katika viwanja vya shule ya msingi Lake Tanganyika wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi.
Mbali na kusisitiza chama hicho kuendelea kuwatumikia wananchi kuwa na maisha bora, amesema hata sasa inajivunia kutekeleza miradi ya maendeleo mingi katika maeneo mbalimbali ya nchi jambo ambalo linawafanya kuingia kwenye uchaguzi wakiwa na sababu za kuwaeleza wananchi.
Dimwa amewaomba wananchi kuendelea kukiamini chama hicho kwa kupiga kura za ndiyo kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi hata kama wamepita bila kupingwa kwenye baadhi ya maeneo yao.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Idd Kimata,amewaomba wananchi kuendelea kujenga imani kwa chama hicho kwa kuwa kina sera imara za kuwahakikishia wananchi maisha mazuri kupitia ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya maendeleo.
Baadhi ya miradi mingi ambayo imetekelezwa na serikali ni pamoja na ujenzi wa shule za misingi, sekondari, Ujenzi wa zahanati,vituo vya afya, hosptali na huduma bora za kitabibu, Barabara za lami, utoaji wa mbolea za ruzuku na sekta ya maji imeimarishwa zaidi.
“Tunaenda kwenye uchaguzi naombeni msifanye makosa. Kama ambavyo mmeendelea kujega imani kwa CCM endeleeni kujenga imani hiyo na msidanganywe” Amesema Kimata.
Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi Mwanamasound Pazi, Amesema kwenye wagombea wa nafasi ya mwenyekiti wa kijiji za halmashauri za mkoa huo vijiji vyenye uchaguzi pekee ni 81, vijiji vyenye uchaguzi wa upinzani ni 49 katika jumla ya vijiji 130.
Mwanamasound amefafanua kuwa wagombea nafasi ya mwenyekiti wa mtaa za manispaa ya Mpanda, Mitaa yenye uchaguzi pekee ni 15, mitaa yenye uchaguzi wa upinzani ni 28 katika jumla ya mitaa 43.
Wagombea wa nafasi ya mwenyekiti wa vitongoji za halmashauri za mkoa wa Katavi kwenye vitongoji venye uchaguzi pekee ni 500, vitongoji yenye uchaguzi wa upinzani ni 162 katika jumla ya vitongoji 662.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili