November 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wahitimu 417 watarajiwa kutunikiwa vyeti ITA

Na Penina Malundo,Timesmajira

JUMLA ya Wahitimu 417 wanatarajia kutunukiwa vyeti na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba katika mahafali ya 17 ya Chuo cha Kodi (ITA)kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Chuo cha ITA,Prof. Isaya Jairo wakati akiongea na waandishi wa habari alisema mgeni rasmi huyo atawatunuku vyeti wanafunzi hao wa Stashahada,Shahada na Stashahada ya Uzamilikwa wahitimu hao  wa mwaka wa masomo 2023/2024.

Amesema kati ya wahitimu hao 417 wahitimu 236 ni wa kiume na wahitimu 181 ni wa kike ambapo wahitimu 195 watatunukiwa cheti cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki yaani the East African Customs and Freight Fowarding Practising Certificate (EACFFPC).

Amesema pia wahitimu 28 watatunukiwa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani Basic Technician Certificate in Customs and Tax Management (CCTM) huku wahitimu 61 watatunukiwa Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani Diploma in Customs and Tax Management(DCTM).

”Wahitimu 119 watatunukiwa Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi yaaniBachelor Degree of Customs and Tax Management (BCTM)na Wahitimu 14 watatunukiwa Stashahada ya Uzamili katikaKodi yaani Postgraduate Diploma in Tanzania,”amesema.

Jairo amesema mahafali hayo yanafanyika wakati chuo hicho kinajivunia mafanikio mengi katika utekelezaji wa mpango mkakati wa tano wa Chuo ambao umejikita katika kutoa mafunzo kwa njia ya kisasa za kidigitali.

”Tayari maandalizi ya kutoa elimu masafa kwa njia ya mtandao yameanza na yanaendelea vizuri ambapo tunatarajia mafunzo ya elimu masafa yatakapoanza yataongeza idadi ya wanafunzi wanaopata mafunzo katika chuo pamoja na kufikia wanafunzi wengi kwa njia rahisi na kwa wakati mmoja na gharama nafuu na kuongeza idadi ya wahitimu,”amesema.

Amesema kufanyika kwa mahafali ni fursa ya kuwapongeza wahitimu pamoja na kutathminimafanikio na shughuli ambazo zinafanywa na Chuo .

Jairo amesema Chuo hicho mahsusi kwaajili ya kutoa mafunzo ya Forodha na Kodi katika ngazi ya Astashahada,Stashahada,Shahada na Shahada ya Uzamili ambapo kinatoa mafunzo yanayoendana na mabadiliko ya sayansi ,teknolojia na uchumi ambayo yanakidhi mahitaji ya soko la wataalamu wanaohitaji katika nyanja ya forodha na kodi hapa nchini,barani Afrika na Ulimwenguni.

Aidha amesema kuwa pamoja na jukumu kubwa la kutoa mafunzo kwa watumishi wa TRA,Chuo cha Kodi pia kinatoa mafunzo na ushauri elekezi kwa wadau wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mamlaka nyingine za Mapato Afrika ikiwemo Zanzibar,Sudan,Botswan na Somalia.