January 29, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tantrade yazindua shindano  la logo ya Made in Tanzania

Na Penina Malundo,Timesmajira

MAMLAKA ya Maendeleo ua Biashara Tanzania (TANTRADE) imezindua shindano la ubunifu wa logo ya  ‘Made in Tanzania’ kwa lengo la kuunda logo itakayotambulika na ya kipekee ambayo itakuwa nembo ya Taifa.

Shindano hilo litashindanisha  kazi mbalimbali za wasanii kwa lengo la kupata nembo ambayo itaitambulisha Tanzania katika bidhaa mbalimbali hasa zinasafirishwa nje ya nchi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mkuu wa Tantrade Latifa Khamis amesema lengo lao ni kuhakikisha bidhaa za Tanzania zinafahamika zaidi si tu katika masoko ya kanda bali pia katika jukwaa la kimataifa.

Amesema logo hii itawakilisha kwa fahari bidhaa na huduma za Tanzania nchini na kimataifa na kuwa  na alama ya ubora,imani na fahari

“Utambulisho huu wa logo wenye nguvu wa chapa utaimarisha ushindani wetu,kuongeza mahitaji ya bidhaa na huduma za Tanzania na kuvutia  uwekezaji katika uchumi wetu.

“Shindano hili linatoa jukwaa la kipekee kwa wabunifu wa picha na wasanii wa Tanzania katika kuunda utambulisho wa taifa letu na kuonyesha bunifu, fahari, na uwezo ulio ndani ya bidhaa na huduma zetu za ndani,”amesema na kuongeza 

“Lengo la shindano hili ni kuunda logo inayotambulika na ya kipekee ambayo itakuwa Nembo ya Taifa letu. Logo hii itawakilisha kwa fahari bidhaa na huduma za Tanzania hapa nchini na kimataifa, na kuwa alama ya ubora, imani, na fahari,lengo letu ni kuhakikisha kuwa bidhaa za Tanzania zinafahamika zaidi,”amesema Latifa.

Amesema Tanzania imefanya maendeleo makubwa katika kuongeza mwonekano wake duniani na kuboresha uhusiano wake wa kibiashara. 

“Licha ya mafanikio yetu mengi,kumekosekana kipengele kimoja,ishara ya taifa inayounganisha na kuwakilisha ubora na upekee wa bidhaa na huduma za Tanzania katika soko la kimataifa,hapa ndipo shindano la Logo ya Made in Tanzania linapolenga kutoa suluhisho.

Amesema utambulisho wa logo utakuwa utambulisho wenye nguvu wa chapa utaimarisha ushindani wetu, kuongeza mahitaji ya bidhaa na huduma za Tanzania, na kuvutia wawekezaji katika uchumi wetu.

“Nawaalika wabunifu wa picha na wasanii, kutoka mikoa yote ya Tanzania kushiriki katika shindano hili la kihistoria,hii ni nafasi yenu ya kuacha alama ya kudumu kwenye mustakabali,”amesema Latifa.

Amesema mwisho kuwasilisha kazi hizo ni Novemba 24 mwaka huu ambapo mshiriki ataruhusiwa kukusanya bunifu zisizochini tati 

Katika shindano hilo  zawadi mbalimbali zitatolewa kwa  wabunifu hao kuanzia  mshindi wa kwanza wa pili hadi watat