November 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Mgomi: Mtakaohitimu TASAF endeleeni kubaki kwenye vikundi

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira,Online Ileje

MKUU wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe Farida Mgomi, amesema wanatarajia kuwaona wale watakaohitimu kwenye Mpango wa Kunusuri Kaya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wanaendelea kuwepo kwenye vikindi, kutokana na vikundi hivyo kuwa na maana kubwa.

DC Mgomi alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanufaika wa Mpango wa TASAF katika Kijiji cha Yuli kilichopo katika Kata la Mlale, wilayani hapa.

Alisema wanatarajia baadhi ya waliomo kwenye mpango watahitimu Septemba 30, mwakani .

” Sasa natamani nikiona mmehitimu tufanye graduation (mahafali), watoto wakihitimu tunaenda kule tunawapelekea mashada, tunawapelekea zawadi na sasa tunataka kuwaona na nyinyi mliokuwa kwenye mpango mwakani mnahitimu kwa sherehe, tunasherehekea neema ambayo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alituletea kwa kipindi mchokuwa kwenye mpango wa TASAF,” alisema DC Mgomi na kuongeza;

Leo mna nyumba bora, mifugo na ninatengea kuwaona wale waliohitimu wanaendelea kuwepo kwenye vikundi sitarajii kuona umehitimu unasema mimi basi, sitaki kuwemo kwenye vikundi, vikundi vina maana kubwa sana.”

Alisema watu wa maendeleo ya jamii wanajua sana umuhimu wa vikundi kuliko yeye, laki wanufaika wa TASAF wameishapata faida za vikundi, ambapo wanaweka akiba, kukopeshana na kuboresha mazingira.

“Ukihitimu kwenye mpango huu usitoke kwenye vikundi na wewe uliyepo kwenye mpango ni muhimu sana kuingia kwenye vikundi , kuna wengine wanasema imani yao, Miungu yao haiwataki kuingia kwenye vikundi .

Lakini Miungu yao hiyo hiyo, imani yao hiyo hiyo inawataka kupokea fedha ya Mama Samia kupitia humo humo, hela kupokea Miungu inakubali, kuingia kwenye vikundi ili mtumie hela yenu kwa pamoja muone mnafanya, Miungu haitaki!

Jamani hapana, tusiwasingizie Miungu ambao hatuwaoni, tusisingizie imani, hakuna imani inayokataa umoja, hakuna imani inayokataa ushirikiano, hakuna imani inayokataa fedha kwa sababu tunapokuwa tunashirikiana kwenye vikundi, maana yake vinatusaidia kiuchumi,” alisema.

Alisema kwenye zile akiba zao inazozunguka ni vema wakaziingiza kwenye miradi ya uzalishaji.

Kwa mujibu wa DC Mgomi wengine wameanza kununua mazao na kuuza ambapo fedha zinakuwa zinaingia za kutosha sio zile za akiba ambazo wanakuwa wamejiwekea.

Aliongeza kwamba anategemea kuona vikundi vinaendelea kuimarika, vinaendelea kutafuta fursa ya kuongeza uzalishaji kama vile ufugaji wa ng’ombe, kuku na nguruwe.

Aliwataka wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya ya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuhakikisha vikundi vyao vinaendeshwa kwa kuzingatia katiba