Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
JAMII imeaswa kuacha tabia ya kuwatelekeza wazazi na badala yake wawatunze ili wapate baraka badala ya kuachiwa laana.
Kauli hiyo imetolewa Novemba 11,2024 na Rais umoja wa mabunge duniani (IPU)na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini,Dkt.Tulia Ackson wakati akikabidhi nyumba za kuishi kwa Wananchi waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu Jijini humo.
Dkt.Tullia amesema kuwa kati ya wananchi waliokabidhiwa nyumba hizo mmoja wapo ana watoto wengine wamefariki na wengine wapo hai wamewaacha katika mazingira magumu kwasababu kama wangekuwa hawana uwezo wangewahudumia kwa kiasi wawezavyo.
“Lakini kuwaacha wazazi na kuwatelekeza sio sawa sawa na ni dhambi kwasababu najaribu kuwaza changamoto hizi sababu naona hili sikuwahi kusikia huko kwingine kwasababu huyo mwingine sikuwahi kumjengea nyumba lakini huyu mwingine tulikuwa tumekarabati nyumba yake yule mtu hatukuwahi kujua kama ana mtoto na tena yupo hapa Mbeya mjini yule Mzee sisi tukaletewa taarifa tukaenda tukakuta mtoto kajaa mle ndani “amesema Dkt.Tulia.
Hata hivyo Dkt.Tulia amesema kuwa haipendezi kutekeleza wazazi na kusema iweje mzazi awe mbaya wakati amewalea vizuri amekuzaa,amekunyonyesha,amekulea huna ujualo na kusema wamekuwa watu wazima wanaona wazazi waathiri maisha yao na kuwa hiyo ni Imani ya uchawi au vyovyote vile wanavyoamini hiyo ni imani potofu na Imani mfu.
Waliokabidhiwa nyumba hizo ambazo zimejengwa na Taasisi yake ya Tulia Trust ni pamoja na Winifrida Kapingu kutoka ya Kata ya Ilemi, Bibi Tusekile Kazimoto na Bibi Mwaine Lumbalile wakazi wa Kata ya Iyunga.
“Sio jambo jema Kama sisi kuwa sehemu ya jamii kuendekeza masuala imani za kishirikina hivyo sasa ndugu zangu mnaonisikiliza hapa tuwakumbuke wazazi wetu na kuwatunza ikiwa ni pamoja na kuwapatia mahitaji yote muhimu unaponiona mimi hapa nami ni mzazi,nami natamani nami siku moja nitumie muda wangu watoto wanitunze ,mzazi aliyekulea toka tumboni mpaka kuwa mtu mzima hawezi kukudhulu “amesema Dkt.Tulia.
Winfrida Kapingu mmoja wa wananchi waliokabidhiwa nyumba na Taasisi ya Dkt.Tulia amesema kuwa amezaliwa upya kwani awali alikuwa analala nje kutokana na nyumba aliyokuwa akiishi kuwa mbovu na kumfanya yeye familia yake kuishi maisha magumu na na ya Mashaka.
Mmoja wa wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo la kukabidhiwa nyumba wananchi hao ,Sophia Yuda amesema kuwa Dkt.Tulia anachofanya kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu ni kitendo cha faraja kubwa na kusema kuwa wapo watu wenye kipato kikubwa lakini kugusa wenye uhitaji ni wachache na katika 100 ,utakuta wawili.
Mpaka Sasa Taasisi ya Tulia Trust ambayo ipo chini ya mkurugenzi wake Dkt.Tulia Ackson ambaye ni Spika wa Bunge na Rsis Umoja wa Mabunge duniani na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini
imejenga nyumba 16 za wananchi wanaoishi katika mazingira ikiwemo mkoa wa Ruvuma .
More Stories
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania
Rais Samia apeleka Bil. 6 kuboresha sekta ya elimu Kaliua
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM