Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Wilaya ya Ilala inatarajia kutoa mikopo ya Halmashauri ya asilimia kumi shilingi bilioni 14, kwa wajasiriamali wadogo wadogo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, katika Kongamano la siku mbili la Wajasiriamali wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
“Tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ,kwa kuruhusu mikopo ya asilimia kumi ambayo aina riba,ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri ambapo awali Serikali ilisitisha mikopo ya Serikali kupitia ngazi ya Halmashauri “alisema Mpogolo.
Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo alisema awali kabla kutoa mikopo hiyo walipita kila kata kutoa elimu ya wajasiriamali wadogo wadogo kila vikundi walipatiwa elimu ya mikopo na taratibu zake.
Mpogolo alisema Halmashauri jiji la Dar es Salaam Halmashauri pekee imepewa kibali na Serikali kutoa mikopo ya Bilioni 14 kwa wajasiriamali ili waweze kukuza mitaji yao ya biashara.
Alisema mikopo hiyo itawakwamua kiuchumi wajasiriamali wadogo wadogo wanawake, vijana na watu Wenye Ulemavu wa wilaya ya Ilala ambao tayari washapatiwa elimu ya mikopo ya Serikali watakopeshwa na kurejesha kwa utaratibu maalum ili wafanyabishara wengine waweze kukopa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Elihuruma Maberya, alisema mwaka jana,Serikal ilisitisha aprili mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia amerejesha mikopo hiyo ambapo alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais kwa mapenzi mema na wajasiriamali
Mkurugenzi Maberya alisema awali mikopo ya Wajasiriamali ilikumbwa na Changamoto Serikali ikasitisha ambapo wafanyabishara mitaji yao ikawa inakufa baada Rais kutambua hilo mikopo ya asilimia kumi inayotolewa ngazi ya Halmashauri Serikali ikarejesha mikopo.
Alisema katika halmashauri kumi za mfano Ilala itatoa mikopo hiyo kupitia taasisi za fedha Benki ambapo katika mwongozo mpya wa mikopo ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ilala inahusika moja kwa moja.
More Stories
Rais Samia kuandika rekodi mkutano G20
Waziri Lukuvi aeleza maono ya Isimani ijayo
Madiwani Korogwe TC wahakikishiwa maji ya uhakika