Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Jumla ya watahiniwa 7176 waliosajiliwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, wataungana na wenzao nchini,kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2024 utakaoanza 11 hadi 29 Novemba 2024.
Kati ya watahiniwa hao watakapofanyia mtihani huo,katika Halmashauri hiyo wavulana ni 3467 na wasichana ni 3709.
Hayo yamebainishwa Novemba 9,2024,katika taarifa iliotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,Violencea Mbakile,alisema watahiniwa 6989 ni wa shule.Kati yao wasichana 3588 na wavulana 3401.
Huku watahiniwa 187 ni wa kujitegemea,kati yao wavulana 66 na wasichana 121.Na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ina jumla ya vituo 60 vilivyosajiliwa kuendesha mtihani wa taifa wa kidato cha nne (CSEE) kwa mwaka 2024.
“Kati ya vituo hivyo 48 ni vya watahiniwa wa shule na vituo 12 ni vya watahiniwa wa kujitegemea.Mkurugenzi Ummy Wayayu, kwa niaba ya uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,amewatakia kila la kheri watahiniwa wote wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2024 na kuwakumbusha kuzingatia na kufuata taratibu zote za mitihani ili waweze kuhitimu salama,”.
More Stories
Waziri Lukuvi aeleza maono ya Isimani ijayo
Madiwani Korogwe TC wahakikishiwa maji ya uhakika
CHADEMA wampongeza Mkurugenzi Mpanda