Na Esther Macha,TimesmajiraOnline, Mbeya
Madiwani na viongozi mbalimbali jijiini Mbeya wameonywa kujiepusha na tabia ya kuingilia majukumu ya wasimamizi wa uchaguzi, kuelekeza uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27,2024.
Kauli hiyo imetolewa Novembe 8,2024 na Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya ,Mohamedi Fakii,wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka kilichofanyika katika halmashauri Kata ya Iwindi Mji mdogo wa Mbalizi Wilaya ya Mbeya.
“Tusiende kuingilia majukumu ya wasimamizi wa uchaguzi, tuwaachie wafanye kazi zao,zipo Wilaya wameonekana viongozi na Madiwani wanaenda kushughulika na masuala ya uchaguzi,niseme hivi msimamizi anakuwa mmoja tu na maofisa wake na timu za uchaguzi.Sisi kazi yetu ni kutoa elimu na kuhimiza namna gani uchaguzi unaenda kufanyika,”amesema .
Fakii amesema,kazi ya uchaguzi wanaopaswa kusemea ni maofisa uchaguzi na msimamizi uchaguzi,ambapo wanaofanya hivyo ni kinyume na wanafanya makosa,kisheria haitakiwi kwani wanaweza kufanyiwa mapingamizi na kukatiwa rufaa.
Aidha amesema kuwa maeneo ambayo yapo pembezoni viwekwe vituo vingi vya kupigia kura,ili kurahisisha watu kujitokeza kwa wingi kupiga kura.TAMISEMI imeongeza vituo vya upigaji kura kwenye maeneo yenye shida ambayo yapo pembezoni na vitawekwa sehemu inayoonekana kwa urahisi.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,Ezekia Shitindi,amesema kazi ya Madiwani ilikuwa kuhamisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari ambao ni wa vyama tofauti na itikadi tofauti .
“Hapa tuna Halmashauri mbili,kazi yetu sisi iliyobaki ni kuhamasisha wananchi wajitokeze Novembe 27, mwaka huu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kuchagua viongozi “amesema Makamu Mwenyekiti huyo.
Maiko Ngailo ni Diwani wa Kata ya Bonde la Songwe Wilaya ya Mbeya,amesema viongozi wanaoingilia ni makosa,kwa sababu wanatakiwa kuwaacha watu wafanye kazi zao. Kuna mipaka na Madiwani wanaoonekana kuingilia waache kwani kila kazi ina mipaka yake,nao wafanye kwa sehemu yao.
More Stories
Waziri Lukuvi aeleza maono ya Isimani ijayo
Madiwani Korogwe TC wahakikishiwa maji ya uhakika
CHADEMA wampongeza Mkurugenzi Mpanda