November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NAOT watakiwa kuendana na viwango vya ukaguzi

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

NAIBU Mkaguzi Mkuu wa Serikali Kuu, Wendy Massoy amewataka wakaguzi kutoka ofisi ya taifa ya ukaguzi (NAOT) kuhakikisha wanaendana na kasi ya mabadiliko ya viwango vya kikaguzi  vya kimataifa katika utayarishaji wa taarifa za fedha za umma. 

Wendy amesema hayo jijini dodoma wakati ufunguzi wa mafunzo ya siku tano yanayoendeshwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) yanayolenga kuimarisha taaluma  na ubora wa ukaguzi kwa watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ili kuhakikisha wanaendana na mabadiliko hayo katika ukaguzi wao.

Amesema Tanzania inaongoza katika masuala ya menejimenti ya fedha za umma kwa mujibu wa Shirikisho la Wahasibu Duniani (IFAC), ikishika nafasi ya kwanza pamoja na Nigeria katika utumiaji wa viwango wa kimataifa vya utayarishaji wa taarifa za fedha za umma ( IPSASs)

Warsha hiyo inajadili masuala muhimu kama viwango vya ukaguzi, utoaji wa taarifa za fedha kwa uadilifu, na matumizi ya viwango vipya vya undelezaji endelevu (sustainability) pamoja na mabadiliko ya kiteknolojia katika fani ya Uhasibu.