Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
RAISĀ Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi mfuko wa mikopo kwa ajili ya kusaidia kuendelezaĀ bunifu na teknolojia zinazobuniwa na vijana wa Kitanzania,ambapo atakabidhi hundi ya Shilingi bilioni 6.3 kwa watafiti 19 na atawatambua na kutoa tuzo maalumu kwa wanasayansi na wabunifu ambao matokeo ya kazi zao yamechangia kuleta mabadiliko ya kiuhumi na kijamii, ndani na nje ya nchi.
Dkt.Samia anatarajia kufanya hayo akiwa mgeni rasmi katika Kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu linalofanyika kila mwaka chini ya uratibu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4,2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam,linalokwenda na Kauli mbiu ya Kongamano kwa mwaka huu kuwa ni”Matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ununifu katika Kuhimili Changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi na Kuchangia kwenye Uchumi Shindaniā.
Hayo yamesemwa jijini hapa leo,Novemba 6,2024 na Waziri Wa Elimu, Sayansi Na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano hilo .
Prof.Mkenda amesema Kongamano hilo linalenga kuwaleta pamoja watafiti, wabunifu, na wadau kutoka sekta mbalimbali, ndani na nje ya nchi ili kujadili kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha mchango wa Sayansi, teknolojia na ubunifu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Amesema kupitia Kongamano hilo Serikali itapata michango ya kisera na kitaalamu ambayo itasaidia kuimarisha sera, mikakati, na juhudi nyingine zinazolenga kuimarisha mchango na mshikamano baina ya taasisi, sekta binafsi, na wadau wa maendeleo katika kuendeleza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kama nyenzo kuu ya kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watanzania.
“ili kufanikisha na kufikia malengo yaliyokusudiwa, nitumie fursa hii kuwaalika Watanzania wote pamoja na wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi, ndani na nje ya nchi, kushiriki Kongamano hili la STICE na hata wale watakaoshindwa kuhudhuria kwasababu tofauti tofauti wafuatulie kongamano hili kwenye luninga kwasababu litakuwa mubashara,
“Ushiriki wenu ni muhimu sana katika kuleta mawazo na mikakati mipya, kuimarisha utafiti na ubunifu, na kuhakikisha kuwa matokeo ya utafiti na ubunifu yanajibu mahitaji na kutatua changamoto za maendeleo ya kiuchumi na kijamii,”amesema Prof.Mkenda.
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo