September 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia apongeza ujenzi jengo la Halmashauri Mbinga

Na Cresensia Kapinga, Timesmajiraonline,Mbinga

RAIS Samia Suluhu Hassan ameridhishwa na ujenzi wa jengo la kisasa la ghorofa moja la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, ambalo limejengwa kwa sh. bilioni 3.3 hadi kukamilika kwake.

Amesema anawashukuru amefika Mbinga kwa madhumuni ya kufungua jengo na amewàpongeza halmashauri hiyo kwa kukamilisha ujenzi huu wa jengo hilo zuri .

Akizundua jengo hilo jana alisema kukamilika kwa jengo hilo ni kutekeleza Ilani ya Chama Cha mapinduzi baada ya kukamilika kwa jengo hilo, wahakikishie huduma zote zinatolewa ndani ya nyumba moja .

“Ni jengo zuri nimeingia ndani kuangalia ujenzi unaridhisha sana na ni jengo lenye nafasi za kutosha kwa hiyo nawashukuru, lakini pamoja na hilo niwapongeze madiwani kwania mmesimamia ujenzi wa jengo hili, lakini pia mmewaza kuwa na jengo la kitega uchumi jengo la kuwawezesha wananchi nimuombe Mungu awatie nguvu na mlimalize jengo hili liweze kufanya kazi iliyokusudiwa,” alisema Rais Samia

” Niwasisitize watakaotumia nyumba hii madhumuni ya Serikali kujenga nyumba hizi ni kuleta mazingira mazuri kwa maofisa wetu wanaofanya kazi ndani ya halmashauri hizi ni kurahisisha utendaji wa kazi kwa hiyo niwaombe sana maofisa wote kutumia majengo haya kwa kutulia na kufanya kazi zenu vizuri kwa kuhudumia wanachi kwa upendo na weledizaidi.”alisema Rais Samia.

Naye Mbunge Jimbo la Mbinga Vijijini, Benaya Kapinga, alisema, wanamshukuru Rais Samia kwa miradi mingi aliyopeleka kwenye jimbo hilo.

Alisema wamepata miradi ya maji sh. bilioni 13.9 , barabara-Amani Makolo-Mbambabay kwa gharama ya sh. bilioni 60, elimu sh. bilioni 10, afya sh. bilioni 2.2 ujenzi wa vituo vya afya sh. bilioni 836 na bilioni 2.8 upande wa barabara.

Alisema kuwa pamoja na fedha zote za miradi yote ya maendeleo waliyopata wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mji huo wa Kiamili kukua kwa kasi jambo ambalo linasababisha huduma ya maji kutotosheleza.

“Mwanzoni wananchi hawakunufaika na madini ya makaa ya mawe, lakini sasa wameanza kupata CSR ila bado wana mang’uniko, makampuni yanapata pesa nyingi kuliko CSR inayopelekwa.

Kahawa bila ruzuku ya mbolea hawavuni .Changamoto ipo bado hawana maghala ya kuhifadhi mazao yao ila bado kuna msululu mkubwa mtaaani,” alisema.

Alisema Kahawa haijauzwa chini ya 4,000 mwaka huu kilo imeuzwa 10,000 hadi 12,000 kwa kilo .

Naye Mbunge wa Viti maalum kupitia vijana, Judith Kapinga na Naibu Waziri Nishati, alimshukuru Rais Samia Suluhu na alimuomba awasaidie kuweka kituo cha Zana za kilimo ili wakulima waweze kuzalisha kwa wingi mazao yao.

Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa alimshukuru Rais kwa kuwajengea jengo zuri lililogharimu sh. bilioni 3.3 , hivyo kusogeza huduma kwa wananchi kwani wameteseka kwa muda mrefu kutafuta huduma za kijamii.

Alitoa sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa shule tatu za kata na ameagiza fedha hizo ziwafike mara moja .

Naye Waziri wa kilimo Hussein Bashe, alisema kuwa Bilioni 10 zimeshalipwa kwa wakulima kuanzia mwaka kesho vituo vyote vya NFRA vitakuwa na mashine za kusafisha mahindi hivyo hakutakuwa na mateso

Alisema mbegu za ruzuku zitaanza kutolewa, hivyo aliwataka wakulima kutowauzia madalali mahindi badala yake wapeleke mahindi Kitengo cha Taifa cha Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, alisema Rais anaenda kuzindua Barabara ya Mbinga -Mbambabay na kwamba kufunguka kwa barabara hiyo kunaenda kuhamsha Ruanda-Ndumbi.

Pia alisema wamepata mkandarasi, hivyo kazi itaendelea. Aidha, alisema barabara Lukuyufusi -Mkenda kuelekea Msumbiji itaanza kujengwa na kwenda kumaliza changamoto hizo.