November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Helios Tower Tanzania yakabidhi maabara ya kompyuta Oljoro

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mwenyekiti wa Almashauri ya wilaya ya Arusha vijijini Ojungu Pinieli Salekwa amezindua maabara ya kompyuta katika shule ya Sekondari Endevesi iliyopo kata ya Oljoro wilaya ya Arusha Vijijini zenye lengo ka kurahisisha njia za ufundishaji kwa wanafunzi wa shuleni hapo.

Kompyuta hizo zimetolewa shuleni kwa ufadhili wa Helios Tower Tanzania kupitia programu yao ya kurudisha kwa jamii ya Connect unconnected ili kuleta maendeleo ya elimu kupitia matumizi ya TEHAMA kwenye mifumo ya elimu Tanzania.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, salekwa amesema kwamba viongizi, wazazi na watoto wa wilayani hapo watakuwa walinzi wa kwanza wa minara hiyo ili elimu ya TEHAMA iwe endelevu

“Lengo la maabara hii (ya kompyuta) ni kurahisisha njia na mbinu za kujifunza bila kutumia muda mrefu (kwa wanafunzi) na kufundishia (kwa waalimu) lakini pia, kuwasogeza karibu na dunia hii ya teknolojia katika mfumo mzima wa kujifunza.”

“Wazizi, viongozi na watoto hawa watakuwa walinzi wa minara yenu.
Mtoto akishajua kwamba hii minara ndiyo imesababisha mimi nikapata computer leo na mimi nasoma
Computer bila mzazi kulazimika kukupandisha roli na bila kulipia chochote kwenda musomea computer unatoka sekondari Unajua computer ni jambo la kuwashukuru helios na camara na ndiyo watakuwa walinzi namba moja”

Leo ukitaka kufanya application yoyote unambiwa ingia kwenye mfumo zamani zilikuja simu za motorola

Naye Gwakisa Stadi, Mkurugenzi Mtendaji wa Helios Tower Tanzania Amesema – ” Lengo la udhamini wa maabara hizi za kompyuta ni kuwaunganisha wanafunzi ambao wanatoka katika jamii za wafungaji ambazo nyingi zipo maeneo ya pembezoni nchini Tanzania, ili kuwa karibu na fusa mbalimbali za kidigitali ambao ni matokeo ya maendeleo ya sayansi na tecknoolojia Duniani”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Camara Education Tanzania, Dayani Mbowe amezisihi kampuni na Taasisi zingine kuendelea kuwekeza katika elimu hasa katika TEHAMA ili kuhakikisha wanaandaa kizazi kinachoendana na mabadiliko ya kisayansi na Teknolojia.

“Tuko hapa endevesi secondary school tunafuraha kubwa leo kuhakikisha kwamba hata shule za pembezoni wanapatiwa huduma hii ya tehama katika elimu, computer 26 smart tv pamoja na projectoer, kufanya ukarabati
Kwenye chumba cha tehama kufunga umeme pamoja na mtandao pia tukafanya mafunzo kwa walimu na viongizi wa shule lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kutumia tehama katika kuboresha ufundishaji”

“Tunahimiza taasisi na kampuni zingine ziwekeze katika elimu hasa katika tehama ili kuhakikisha tunaandaa kizazi chetu kuendana na mabadiliko ya kisayansi na teknolojia duniani”

Mkuu wa Shule hiyo, Godson Sukrueti amesema mradi huo unafaida kwao na kwa wanafunzi kwa ujumla kwani utaondoka changamoto iliyokuwepo awali ya upatikanaji wa vitabu shuleni hapo.

“Mradi huo unafaida kwetu sisi walimu
Pamoja na wanafunzi wetu kwasababu sisi walimu itatusaidia kwanza kuweza kurahisisha suala zima la ufundishaji lakini kwa wnafunzi wetu katika ujifunzaji

“Tumekuwa na tatizo la vitabu lakini kwasababu ya huu mradi mliotuletea wanafunzi wetu wanaweza kupata material mbalimbali kwenye hizi computer na walimu wanaweza wakatuma material mbalimbali na wanafunzi wakaweza kuyapata kupitia computer hizi”

Mwanafunzi wa shule hiyo Mwanahamisi Rajab aliwashukuru wadau hao kwa kuwaletea vifaa hivyo kwani utawasaidia katika usomaji na kupelekea kuwa na matokeo mazuri kuanzia sasa na siku zijazo.

Naye Daud Lashine mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo amesema kutokana na uhaba wa vitabu shuleni hapo, vifaa hivyo vitawasaidia kupata vitabu hivyo mtandaoni na kujiendeleza vyema katika masomo yao.