September 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia kuanza ziaraya siku sita Ruvuma leo

Na Cresensia Kapinga, Timesmajiraonline, Songea

RAIS Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuanza ziara ya kikazi siku sita kuanzia Leo Septemba 23, mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana.

Alisem Rais akiwa mkoani humo matukio matatu yatafanyika ambapo tukio la kwanza atafunga Tamasha la tatu la Taifa la Utamaduni ambalo kilele chake ni leo.

Alifafanua kuwa Septemba 24 mwaka huu ataanza ziara ya kikazi ambapo atazitembelea wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma.

Alitaja Wilaya hizo kuwa Mbinga,Nyasa,Tunduru, Namtumbo na Songea na kwamba atafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuongea na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.

Mkuu wa Mkoa Ahmed Abbas Ahmed alisema pia Rais Samia, atazindua,K kufungua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuongea na wazee wa Mkoa wa Ruvuma.

Alieleza kuwa tukio la tatu ambalo litafanyika ni kushiriki Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) Taifa linalotarajia kufanyika katika Manispaa ya Songea ambapo Rais baada ya kuhudhuria atafunga kikao hicho kinachotarajiwa kufanyika Septemba 28 mwaka huu ambacho kitahudhuriwa na wajumbe wa umoja wa wanawake wa wilaya zote hapa nchini.

“Kama nilivyosema baada ya kufungwa kwa mkutano wa UWT Taifa Rais Samia atahitimisha ziara yake mkoani Ruvuma kwa kufanya mkutano wa hadhara wa wananchi wa manispaa ya Songea katika uwanja wa Majimaji ambapo atatumia mkutano huo kuongea na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma”alisema.

Alisema kuwa ziara hiyo ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma hivyo pamoja na mambo mengine aliwaasa kuboresha mazingira ili yawe rafiki jambo ambalo litawavutia wageni mbalimbali ambao wanatarajia kuwasili mkoani humo.

.

“Tunajua