September 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wazazi Jakaya Kikwete wafanya usafi Kituo cha afya Segerea

Na mwandishi wetu, TimesMajira Online

JUMUIYA ya Wazazi ya chama cha Mapinduzi Tawi la Jakaya Kikwete segerea wamefanya usafi katika kituo cha afya Segerea wakiongozwa na Mwenyekiti wa kata ya Segerea wa Jumuiya ya Wazazi Abdalah Loko pamoja na Kamati ya Utekelezaji Jakaya Kikwete

akizungumza mara baada kumaliza kufanya usafi Katibu wa Wazazi Jakaya kikwete HERI SHAABAN,moja ya jukumu la Jumuiya ya Wazazi ya CCM kusimamia sekta afya ,Sekta ya Elimu na Mazingira.

“Tumepokea maelekezo ya viongozi wetu wa ngazi ya kata ambayo yametoka wilayani tushiriki katika kazi za kijamii kwa ikiwemo kuandaa mkutano mkuu wa tawi na wanachama ambapo Jumuiya yetu kwa kushirikiana na Kamati ya utekelezaji tumejipanga vizuri katika kukamilisha mikakati yetu “alisema Heri

Aidha alisema mikakati mingine waliopanga kwa kushirikiana na Kamati ya utekelezaji ya tawi kuongeza wanachama wapya kuwasajili katika mfumo wa kadi za kisasa za electonic pamoja na kujisajili katika Daftari la mpiga kura.