Na Mwandishi wetu ,TimesMajira,Online
MATOKEO ya Kura za maoni kwa nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA )yametangazwa rasmi na Tundu Lissu kushinda nafasi hiyo kwa kura 405.
Katika kikao kilichokaliwa leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na Baraza kuu la Chadema limeweza kupiga kura na kumchagua Lissu kushika fimbo ya urais kwa Chama hicho.
Wengine waliogombea na Lissu ni Lazaro Nyalandu ambae amepata kura 36 na Dkt Maryrose Mjinge amepata kura moja.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako