October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TALGWU Mara wampa tano Samia watumishi kulipwa mishahara Hazina

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira, Mara

Wafanya kazi wa Serikali za mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Mara wameeleza kuridhishwa na hatua ya Serikali kuwahamisha watumishi hao kulipwa mishahara yao kupitia hazina badala ya kupitia mapato ya ndani ilivyokuwa awali kwani kufanya hivyo nikurejesha ali ya utumishi kwa taifa lao.

Akizungumza na wandishi wa habari Mwenyekiti wa Talgwu Mkoa wa Mara Dkt. .Magreth Shaku, ameungana na katibu Mkuu wa TALGHU Taifa kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan,ambapo baada ya Muda mrefu Serikali imewahamishia watumishi 465 kati ya watumishi 645 wa serikali za mitaa kulipwa mishahara kupitia mfuko Mkuu wa Serikali (Hazina) Jambo ambalo linatajwa kurejesha molari katika utumishi.

Shaku alisema Mkoa wa Mara ni watumishi 16 wamebahatika kuingia katika mfumo huo wa malipo ambapo sasa wanaamini watumishi ambao walikuwa hawapati huduma ya Bima ya Afya sasa watatibiwa tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma pamoja na uhakika wa Kupata mafao yao baada yakustaafu.

“Tunaahidi sasa utumishi bora sisi kwa mkoa wa Mara kutokana nanamna Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa msikivu kwa watumishi wake nahili ni jambo ambalo lilikuwa gumu kwa muda mrefu, lakini sasa limerejesha furaha zaidi,” Dkt. Shaku Mwenyekiti wa Talgwu mara.

Aidha baadhi ya watumishi walisema awali hali ilikuwa mbaya kwani watumishi walikuwa wakicheleweshewa mishahara nakusbabisha kuingia katika mikopo isiyo ya lazima lakini kuingizwa katika Malipo ya Mfuko wa serikali itaenda kubadilisha maisha ya watumishi hao.