September 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watakaofanya ununuzi nje ya Mfumo wa NeST kufungwa jela

Na Mwandishi Wetu

WATUMISHI wa Serikali watakaofanya ununuzi wa Umma nje ya Mfumo wa NeST watakuwa wamefanya kosa la jinai, na kukabiliwa na adhabu ya kifungo jela pamoja na kulipa faini, kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023.

Akizungumza kwenye kipindi maalum cha Tenda Radio, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Wakili Paul Kadushi, amewataka viongozi wa taasisi za serikali na watumishi kwa ujumla kuzingatia matakwa ya sheria hiyo iliyoanza kutumika Juni 17, 2024 na kanuni zake ambazo zimeanza kutumika Julai 1, 2024.

Kadushi amefafanua kuwa sheria iliyofutwa haikuweka ulazima wa kutumia mfumo wa kielektroniki kufanya ununuzi, hatua iliyosababisha taasisi nyingi kufanya ununuzi nje ya mfumo.

“Lakini kwa sheria hii mpya [Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023] sasa imeweka sharti la lazima kwa taasisi nunuzi zote kutumia mfumo wa kielektroniki katika kufanya ununuzi,” Wakili Kadushi aliiambia Tenda Radio.