Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Katavi
RAIS Dk Samia Suluhu Samia amesema Bandari ya Kalema iliyopo kwenye Ziwa Tanganyikani imekaa kimkakati na pia kitovu cha biashara kati ya mataifa ya Tanzania, Jamhuri ya Kongo, Zambia na Burundi.
“Ninafahamu Bandari ya Karema ni kiungo muhimu cha kibiashara kwani kinachochea ukuaji na maendeleo ya uchumi na kijamii kwa watu wa mataifa ya Tanzania, DRC, Zambia na Burundi,” alisisitiza Rais Samia.
Akizungumza kwenye Sherehe za Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi zilizofanyika kitaifa mkoani Katavi, Rais Samia alisema anatambua pia kilio cha wana-Katavi cha kununuliwa meli kwani atasema neno baada ya kukamilika uundwaji meli alizoahidi maeneo mengine nchini.
“Serikali yangu itafanya kila linalowekana kuhakisha kuwa Bandari ya Karema mbali ya kuwa eneo kiunganishi na mataifa tajwa itaendelea pia kuwa kitovu cha biashara,” alisema na kuongeza anaelewa umuhimu wa eneo hilo kimkakati.
Rais Samia alieza pia sabubu ya kusimamisha shughuli zote uvuvi katika Ziwa Tanganyika kwa muda wa miezi mitatu ili kutoa nafasi kwa samaki kuzaliana, kwani walianza kutoweka kwenye ziwa hilo.
“Watalaamu waliona upungufu na kutoweka kwa samaki katika ziwa Tanganyika na hivyo wakakubaliana nchi nyingine wadau wa ziwa hilo kusimamisha shughuli za uvuvi kwa kipindi cha miezi mitatu,” alisema.
Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imefanya uwekezaji mkubwa wa kiasi cha shilingi bilioni 47.6 kuifanya kuwa bandari ya kisasa zaidi kuliko bandari zote zilipo kwenye maziwa Victoria na Nyasa.
Maboresho ya Bandari ya kimkakati ya Karema ulianza mwaka 2019 na kukamilika mwaka 2022 kwa sasa inafanya kazi kwa muda masaa 24 na inafaa vyote vya kisasa. Kutoka Bandari ya Karema hadi Bandari ya Kalemie nchini DRC ni umbali kilomita 338 na Bandari ya Moba pia DRC ni Kilomita 298.
Kwa mujibu wa taarifa ya TPA, Bandari ya Karema imeleta mageuzi makubwa katika usafiri na usafirishaji wa mizigo kwani huduma zote zinazotolewa bandarini hapo ni za kisasa na zinakidhi matakwa ya watumiaji.
Ziwa Tanganyika lenye urefu wa kilomita 673, upana wa kilomita 72 na kina cha ujazo (cover surface) cha meta (SQM)32,893. Nchi nne za Tanzania, DRC, Zambia na Burundi zipo sehemu ya ziwa ambapo Tanzania ina asilimia 41 ipo Tanzania na asilimia 45 ipo sehemu ya DRC.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi