September 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bonnah ashangaa mazingira machafu Kimanga

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli ameshangazwa na mazingira machafu ya mtaro wa maji ya mvua Mtaa wa Kimanga wilayani Ilala huku viongozi wa eneo hilo kushindwa kuchukua hatua.

Bonnah wakati wa kukagua miradi ya maendeleo alifanya ziara Mtaa wa Kimanga katika mradi wa mifereji na kukuta mfereji wa maji ya mvua mchafu ambapo alitoa agizo kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Abdalah Lumungwi Jumamosi ya Julai 20,2024 ashiriki usafi wa pamoja wa kusafisha mtaro pamoja na Mbunge.

“Mwenyekiti umeshindwa kuchukua hatua za kusafisha na wananchi wako Jumamosi nitakuja kushiriki usafi asubuhi nataka mtaro huu uwe msafi wananchi wasipatwe na magonjwa ya mlipuko,” amesema Bonah.

Katika ziara hiyo alikagua eneo la kujenga zahanati,soko,kivuko cha watembea kwa miguu mtaa Twiga na matundu ya vyoo na baadae mkutano wa hadara.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Abdalah Lumungwi amesema wananchi wa eneo hilo wamekuwa wazito katika suala la utunzaji mazingira.