Na Joyce Kasiki,Timesmajira online
MAMLAKA ya Serikali Mtandao (eGA) imeendelea kuwasihi wananchi kutumia mfumo wa e-mrejesho katika kuwasiliana na serikali kwa kutoa hoja zao ili Serikali iweze kuzifanyia kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la eGA kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) jijini Dar Dalaam Meneja Mawasiliano wa eGA Subira Kaswaga amesema mfumo huo umejengwa ili uwe kama daraja litakalowezesha mwananchi mmojammoja kuwasiliana na serikali na kusikilizwa hoja yake na kufanyiwa kazi.
Amesema , suala la kujenga mifumo kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi katika utumishi wa umma ni jukumu la eGA huku akisema katika jukumu hilo imejengwa mfumo wa e mrejesho ambao ni daraja la.mawasiliano batons ya wananchi na Serikali
Kaswaga amesema kupitia mfumo huo, wananchi wanaweza kuelezea kero,changamoto yoyote ,maoni ,kuuliza swali lolote au hata kupongeza Serikali na mambo yote kwa pamoja yakafanyiwa kazi na Serikali
“Mfumo unapatikana kwa njia ya simu ya mkononi kwa kubonyeza *152*00# halafu namba 9 na kuendelea kufuata maelekezo na taasisi zote za Umma zimeunganishwa katika mfumo huu wa e-mrejesho,kwa hiyo mwananchi akiwa na kero mbalimbali anaweza kuwasiliana na Serikali ikazifanyia kazi.”amesema Kaswaga
Kwa mujibu wa Kaswaga huduma hiyo inapatikana kwa kupakua app ya e-mrejesho au kwa kutumia tovuti ya www.emrejesho.co.go.tz,
Aidha amesema kutokana na utendaji wake,mfumo huo umetambuliwa kimataifa kwamba ni jukwaa huru ambalo linawasaidia wananchi kuwasiliana na serikali na kupitia mfumo huo eva inaweza kushindwa tuzo katika Umoja wa Mataifa ya ubunifu wa huduma za umma mwaka huu 2024 ambazo zilitolewa nchini Korea.
“Kwa hiyo nitoe rai kwa wananchi kuutumia lakini pia taasisi za umma zihamasishe wadau wake kwa maana ya wananchi wanaowapa zile huduma watumie zaidi mfumo wa e mrejesho kuwasilisha maoni yao.”amesisitiza Kaswaga
Vile vilenameaema taasisi hiyo pia imejenga mfumo wa kubadilishana taarifa serikalini kwa maana ya mifumo kusoma kwa lengo la kurahisisha na kuboresha uwajibikaji seeikalini.
“Kama tumavyofahamu kwamba mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza taasisi za umma kubadilishana taarifa kidigiti , kwa hiyo sisi kama mamlaka tumetengeneza mfumo huo na tayari tumeshaunganisha mifumo mbalimbali na sasa wanachokifanya ni kuzihamasisha taasisi za umma ziweze kujiunga na mfumo huo ili ziweze kubadilishana taarifa.”
Kwa mujibu wa Kaswaga mpaka sasa taasisi ambazo zimeunganishwa na mfumo huu ni taasisi 141 na mifumo 148 imeshaunganishwa na katika hiyo mifumo 109 inasomana na kubadilishana taarifa.
“Kwa hiyo tunafanya jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na ofisi za umma ambapo July 22-29 wanatarajia kuwa na kikao na taasisi za umma taktiban 70 kwa lengo la kuwapa elimu kuhusiana na mfumo huo lakini pia kuunganisha ili hizo taasisi zijiunge na mfumo huo.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba