Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online, Makambako
MASHINDANO ya kugombea Kombe la Mpapai (Mpapai Cup), yanaanza kutimua vumbi kesho katika Wilaya ya Makambako mkoani Iringa.
Lengo la kuafnyika kwa mashindano hayo ni, kuelimisha umma juu ya kupiga vita mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), huku yakitarajiwa kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali.
Mpapai Cup yameandaliwa na Tabibu Bingwa wa Tiba Asili, Mbadala Dkt. Haji na yamepangwa kufanyika katika Uwanja wa Polisi mjini Makambako ambapo wapenzi wa soka wameombwa kujitokeza kwa wingi.
Aidha, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Salum Madadi ameyapongeza mashindano hayo.
Akizungumzia mashindano hayo, Madadi amesema wakati huu wa Mapumziko ya Ligi Kuu, wananchi wamekuwa wakipata burudani kwa mechi za mitaani.
Alisema, amevutiwa zaidi na michuano ya Mpapai Cup ya kupiga vita mauaji ya watu wenye ulimavu wa ngozi (Albino).
“Ni ujumbe mzuri na kila mtu anajua kadhia inayowapata ndugu zetu Albino, nampongeza sana muaandaaji wa michuano ya Mpapai Cup,” amesema Madadi.
Hata hivyo amesema, Dkt. Haji Mpapai ameonesha uungwana na kujali watu wenye ulemavu wa ngozi hivyo kama viongozi wa mpira nchini tunatoa ushirikiano.
Timu sita zinatarajiwa kuchuana katika michuano hiyo, ambazo zimepangwa katika makundi mawili A na B.
Timu zilizopo katika kundi A ni Bodaboda FC, African Kids na Lyamkena FC, na kundi B lina timu za Bajaji FC, Chama la wana na Makambako Grace.
Mechi ya ufunguzi itachezwa katika uwanja wa Polisi Mjini Makambako itakuwa kati ya Bajaj FC na African Kids
Kauli mbiu ya mashindano hayo ni kataa mila potofu pinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vitendo vya kikatili watanzania ni wamoja michezo hutuweka pamoja zaidi.
More Stories
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship
Mnzava apania kuwapeleka vijana Simba na Yanga