Na Joyce Kasiki,Dar Es Salaam
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema inakwenda kuwekeza nguvu kubwa kwenye kuelimisha wafanyabiashara (walipa kodi) hasa kuijua sheria ya kodi ya 2024/2025
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maoneaho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) jijini Dar es Salaam,Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa TRA Hudson Kamoga,amesema hatua hiyo itamwezesha mlipa kodi , kulipa kodi bila shuruti.
Amesema pia TRA itahakikisha inatumia mifumo zaidi katika shughuli zake ili kurahisisha hufuma kwa wateja kwa wake.
Kamoga ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wafanyabiashara kutunza kumbukumbu kwa kutoa risiti za mashine (EFD) kila wanapofanya mauzo .
“Kuanzia mwezi wa kwanza mpaka wa tatu huwa tunafanya makadirio ya biashara,changamoto kubwa tunayokutana nayo,ni namna wafanyabiashara wanavyotunza kumbukumbu,Tiba ya utunzaji kumbukumbu ni kutoa risiti za EFD ambapo inapunguza kwa kiasi kikubwa sana ugomvi kati ya mlipa kodi na Afisa wa Mamlaka,
“Kwa hiyo nitoe wito ,wafanyabiashara tuendelee kutimiza wajibu wetu wa kutoa risiti za EFD kila tunapofanya mauzo ya bidhaa au kutoa huduma,lakini pia wananchi tuwe na msukumo mkubwa wa kudai risiti ya EFD yenye thamani sawa na kile ulichotoa ili kutuwekea ulinzi binafsi maana unaweza ukakuta anakimbiza mwizi, wewe ukakutwa na vitu ukaulizwa hii umetoka wapi utakaposema umenunua itabidi uoneshe risiti,kwa hiyo risiti ni moja ya ulinzi wako hivyo ni muhimu kuwa na risiti kila unaponunua.”amesisitiza Kamoga
Vile vile amewataka wananchi wadai risiti yenye thamani ya fedha halisi kila wanunuapo bidhaa ili seeikali iweze kukusanya kodi na kujenga miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Katika hatua nyingine amesema ili kumlinda mtanzania,TRA imeweka mfumo wa hakiki stempu mfumo ambao upo kwenye bidhaa mbalimbali vikiwemo vinywaji kwa lengo la kudhibiti vinywaji ipo kwenye bidhaa mbalimbali zikiwemoa vinywaji ,hii ni moja kati ya njia za kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki.
“Nawaomba watanzania wenzangu kutunza na kujali afya zetu tumia kinywaji ambacho umehakiki stempu yake, hakikisha ile stempu ni ‘originali’ halisi iliyopo kwenye kinywaji kwa kupakua ‘application ‘ ya hakiki stempu, kwa hiyo ukichukua ile ‘application ‘ ukiweka kwenye kinywaji ntakwambia kama ni halisi au la.” Amesema Kamoga
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi