Na Doreen Aloyce, Dodona
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charlse Kichere ametoa taarifa yake kuhusu ripoti ya mwaka wa fedha ulioishia juni 30, 2019 huku akieleza ubadhilifu wa fedha uliobainika katika taasisi za serikali, vyama vya siasa na mashirika ya umma.
Akiwakilisha ripoti hiyo jana jijini Dodoma mbele ya waandishi wa habari alisema jumla ya hati 1082 za ukaguzi zilibaini kuwepo kwa hati zinazoridhisha 1,017 (asilimia 94), hati zenye shaka 46(asilimia 4.25) huku zisizoridhisha ni 7(asilimia 0.64).
Akifafanua ripoti hiyo ya mwaka wa fedha 2018/19 ambayo iliwsilishwa Bungeni aprili 2 mwaka huu . Alisema jumla ya hati 275 zilikaguliwa Serikali Kuu, hati zinazoridhisha 250 ,hati zenye shaka 23, na hati zisizoridhisha 2.
Mamlaka ya serikali za Mitaa, hati zilizokagukiwa ni 185, ambapo safi ni 176, zenye shaka 9, hakuna chafu, kwa mashirika ya Umma zilikaguliwa hati 148 zikiwa na hati zinazoridhisha 147,hati zenye shaka hakuna na zisizoridjisha 1.
Miradi ya maendeleo hati zilizokaguliwa 455 ambazo zina hati zinazoridhisha 441,zenye shaka 13, na zisizoridhisha 1, Vyama vya siasa zilizokaguliwa ni 19 zikiwa na hati zinazoridhisha 3 ,zenye shaka 1 na zisizoridhisha 3 pamoja na hati mbaya 12.
Alizitaja Taasisi zisizoridhisha kuwa ni ubalozi wa Tanzania Addis Ababa,kampuni ya Stamigold, Tume ya Taifa ya mpango wa utumiaji bora wa ardhi,mradi wa programu ya maendeleo ya sekta ya maji katika Halmashauri ya Handeni.
Pia alivibainisha vyama vya siasa vilivyopata hati yenye shaka na hati isiyoridhisha na hati mbaya ambavyo ni Alliance for Africa Farmers Party, African Democratic Alliance (ADA TADEA),chama cha ukombozi wa Umma (CHAUMMA) ,Demokrasia Makini ,Democratic Party, National Reconstruction Alliance,Alliance for Democratic Change ,Chama cha sauti cha umma (SAU).
Vingine ni United democratic part (UDP),united people’s democratic part ,Tanzania labour part ,union for Multipart democracy (UMD) ,the National convetion for construction and Reform Mageuzi(NCCR -Mageuzi) ,Civic united front (CUF),National League for Democracy (NLD) na Chama cha kijamii (CCK).
USIMAMIZI WA MAPATO YATOKANAYO NA KODI.
Akizungumzia kuhusu usimamizi wa mapato yatokanayo na kodi katika mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 jini 2019 Kichere alisema mamlaka ya mapato Tanzania ilikusanya kiasi cha shilingi trilioni 15.74 kati ya makisio ya shilingi trilioni 18.29 hivyo kutofikia malengo kea kiasi cha shilingi trilioni 2.55 sawa na asilimia 14.
Aidha aliongeza jumla hiyo ya makusanyo haihusishi shilingi bilionu 20.05 za vocha za misamaha ya kodi na fedha za marejesho ya kodi kutoka hazina.
“Mapato halisi ya mwaka wa fedha 2018/19 yakijumuisha vocha za misamaha na marejesho ya kodi ni shilingi trilioni 15.76 ukilinganisha na makusanyinyo halisi ya mwaka uliopita 2017/18 ambayo ni shilingi trilioni 15.40 ambapo kuna ongezeko la shilingi bilioni 360 sawa na asilimia mbili”alisema.
Pamoja na mambo mengine alisema taarifa hiyo imebaini maeneo yafuatayo yatakayosaidia katika kuongeza mapato ya serikali ili kufikia malengo yaliyowekwa endapo yatafanyiwa kazi kwa haraka ;
KODI ZINAZOSUBIRI MAAMUZI YA MAMLAKA ZA RUFAA ZA KODI:
Katika mwaka ulioishia tarehe 30 juni 2019 mamlaka ya mapato tanzania ilikuwa na mashauri ya kodi kwenye mamlaka za rufaa za kodi ya kiasi cha shilingi trilioni 366.04.
Hata hivyo kiasi hicho kuwa nimepungua kwa asilimia 4.6 ikilinganishwa na mwaka uliopita 2017/18 ambapo kulikuwa na mashauri ya kodi ya kiasi cha shilingi trilioni 382.71
MAPUNGUFU KATIKA KUSIMAMIA PINGAMIZI ZA KODI
Kuhusiana na mapungufu katika kusimamia pingamizi za kodi alisema Mamlaka ya mapato imekubali pingamizi za kodi zinazofikia shilingi bilioni 84.62 zilizowasilishwa na walipa kodi mbalimbali na kwamba pingamizi hizo huchelewa kufanyiwa kazi kinyume na utaratibu wa TRA wa huduma kwa mteja ambapo ucheleweshwaji huo una madhara katika kufikia malengo ya makusanyo kwani kodi ua thamani hiyo inakiwa haijalipwa mpaka uamuzi wa pingamizi hizo utolewe.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge hesabu za serikali (PAC) Naghenjwa Kaboyoka alisema kuwa mashirika yanayocheza na pesa ya umma watakaa na CAG na vyombo vya habari waangalie wale waliofanya makusudi watapelekwa kwa Mh.Rais ili hatua dhidi yao zichukuliwe.
Alisema wapo baadhi ya wakurugenzi wa mamlaka ambao uwaondoa wakaguzi wa ndani wakijua kuwa wanatoa taarifa hivyo na kupelekea watendaji hao kuwapeleka pembezoni ili kiwaziba midomo .
Kuwa watakapo kaa watajadili na wataangalia njia bora za kuwalinda ili fedha za umma zisipotee.
Nae alisema Abdala Chikota makamu mwenyekiti kamati ya kudumu ya bunge ya serikali za mitaa (LAAC) alisema kuwa bado ku a changamoto kwenye mamlaka ya serikali za mitaa ambapo bado wapo baadhi ya maafsa utumishi ambao bado ufanya kazi kwa mazoea .
Kuwa wapo ambao wanawalipa watumishi hewa huku akisema zile Hamlashauri ambazo ufanya kazi kwa mazoea ziwezw kuhojiwa zaidi..
More Stories
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha