November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jukwaa la Wanawake Ubungo yaanza ziara za Kata

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

JUKWAA la uwezeshaji Wanawake Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam, leo Mei 11, 2024, limeanza ziara ya Kata kwa Kata kwa ajili ya kukagua uongozi wa jukwaa hilo.

Ziara hiyo ilianza Kata ya Kibamba, kwa lengo la kutoa semina kwa Viongozi wa Majukwaa kuhusu utendaji wao bila kuingilia Majukumu mengine.

Lakini pia, kuwaeleza viongozi Majukumu ya Jukwaa la Wanawake na makundi Maalum, ambapo elimu hiyo ilitolewa na Saida Bawazir Kaimu Katibu wa Jukwaa Wilaya ya Ubungo.

Akiongea na viongozi wa jukwaa hilo Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wilaya ya Ubungo, Mariam Kawawa amewasisitiza kusimama na Jukwaa pamoja na kujisajili katika program ya IMASA.

Program hiyo ipo chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni mahsusi kwa kuimarisha uchumi wa Wanawake na makundi Maalum.

Hata hivyo viongozi hao walipatiwa Elimu ya malezi, makuzi na unyanyasaji wa kijinsi sambamba na kusajiliwa katika Mfumo wa IMASA kutoka kwa maafisa wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Diwani Kata ya Kibamba, Peter Ikamba pamoja na wajumbe wa Serikali ya Mitaa yote ya Kata hiyo.