Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), lina mchango mkubwa wa utunzaji wa misitu ndani ya Hifadhi za Taifa 21 zinazosimamiwa na shirika hilo, jambo ambalo limechangia kupunguza Hewa ya Ukaa ambayo ni chanzo kikuu cha uchafuzi wa Mazingira.
Uchafuzi wa mazingira unapelekea Mabadiliko ya tabianchi yanayoikumba dunia kwa sasa. Hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kutunza mazingira ili dunia iwe ni eneo salama kwa kuishi kwa ajili ya binadamu na wanyamapori.
Hayo yamesemwa na Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara TANAPA, Massana Mwishawa akiwa katika Maonesho ya siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.
Aidha, Naibu Kamishna Mwishawa, amewataka TANAPA wanaoshiriki maonesho hayo kutoa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa Mazingira ili maeneo hayo ya Hifadhi za Taifa yaendelee Kuwa na mchango katika sekta hizo.
TANAPA ni taasisi kinara kwenye utunzaji wa Mazingira ambao unamchango mkubwa katika sekta ya Maliasili, Nishati, Kilimo na Uvuvi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa