Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KAMPENI maarufu ya ‘VOTE NOW’ inayoendeshwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), kuzipigia kura Hifadhi ya Taifa Serengeti kuwa Hifadhi bora Barani Afrika na Kilimanjaro kuwa Kivutio bora cha utalii barani Afrika kwa mwaka 2024 imetia nanga katika Maonesho ya Wizara ya Maliasili na Utalii yanayoendelea katika viwanja vya Bunge Jijini, Dodoma
Zoezi hilo la ‘VOTE NOW’, limewavutia wabunge wengi na wageni wanaotembelea bunge kusikiliza mijadala mbalimbali na kushiriki kupiga kura ili hifadhi hizo ziweze kushinda.
Ushindi huo utazifanya hifadhi ya Serengeti na Mlima Kilimajaro ziweze kujulikana kimataifa na kuvutia watalii wengi kuja kuzitembelea na kuongeza mapato kwa Taifa.
Katika hatua nyingine wabunge na wageni hao wamefurahishwa na kuridhishwa na hamasa zinazotolewa na TANAPA ili kufanikisha zoezi la VOTE NOW na kuahidi kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawajapiga kura ili wapige kwa wingi kabla ya kuhitimishwa kwa zoezi hilo Septemba, mwaka huu.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa