November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waathirika maporomoko ya Hanang waishukuru serikali

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

WAATHIRIKA wa maporomoko ya maji na tope, wameishukuru serikali kwa jitihada wanazozifanya ikiwemo msaada wa tiba ya kisaikolojia ili kuwanusuru na hali waliyonayo kwa sasa.

Maporomoko hayo yalitokea katika kijiji cha Ganana wilayani Hanang mkoa wa Manyara, ambapo baadhi yao wakiwemo wanafunzi waliopoteza wazazi na kupata athari ya afya ya akili kutokana na msongo wa mawazo.

Mwalimu Yusufu (aliyekalia kiti), akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Gendabi waliokumbwa na maporomoko ya mlima Hanang kama sehemu ya kuwapa faraja kutokana na madhira yaliyowapata.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ganana, Maiko Henda amesema baadhi ya changamoto zinazowakabili kwa sasa ni afya ya akili kutokana na wahanga wengi wengi kupoteza wazazi, ndugu na mali.

Aidha, Serikali imeendelea kutoa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo kutuma timu za wataalamu wakiwemo wa tiba na saikolojia kutoka Wizara ya Afya na Tamisemi.

Lengo ni kufanya tathimini ya athari zilizojitokeza pamoja na utoaji wa elimu kuhusu masuala mbalimbali kwa waathirika hao.