Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
WIZARA ya Maliasili na Utalii imefanikiwa kuanza utekelezaji wa Uwekezaji Mahiri kwenye Maeneo ya Wanyamapori (Special Wildlife Investment Concession Areas – SWICA) ambapo jumla ya Dola za Marekani 2,773,000 sawa na Shillingi bilioni 7.1 zimepatikana ikiwa ni ada ya vitalu zilizokusanywa tangu kusainiwa kwa mkataba tarehe 3 Januari, 2024.
Hayo yamesemwa jijini hapa leo,Mei 31,2024 Bungeni na Waziri wa Wizara hiyo Angellah Kairuki wakati akiwasilisha Makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 ambapo hatua hiyo ni kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za utali nchini.
Ambapo amesema kupitia Uwekezaji huo Wizara yake inategemea kuongeza mapato kufikia Dola za Marekani millioni 312 sawa na wastani wa Dola za Marekani millioni 15.5 kwa mwaka.
“Tanzania imefanikiwa kuingia katika kundi la kwanza (Category I) la nchi wanachama zenye Sheria zinazotekeleza Mkataba wa CITES kikamilifu hatua inayotajwa kuiwezesha Tanzania kufanya biashara ya uwindaji wa kitalii na mataifa ambayo masharti ya kupokea nyara kutoka kwenye nchi ambazo Sheria zake ziko katika kundi la kwanza,”amesema Kairuki.
Pia amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imefanikiwa kupandisha hadhi Eneo la Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara, lenye hadhi ya Urithi wa Dunia kuwa miongoni mwa maeneo yenye mahusiano ya kisayansi kati ya binadamu na mazingira (Man and Biosphere Reserve).
Amesema hadhi hiyo imetolewa na UNESCO mwezi Julai, 2023 na hivyo kuongeza idadi ya maeneo yenye sifa hiyo kutoka 5 hadi 6 na hatua inayotajwa kuchochea shughuli za utalii wa malikale kwa kuongeza idadi ya watalii wa Kimataifa katika eneo la Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara hususani kupitia utalii wa meli.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi