November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Asilimia 40 walioambukizwa Covid-19 hawana dalili

na Mwandishi Wetu

KITUO cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) Marekani kimedokeza kwamba karibu asilimia arobaini 40 ya watu walioambukizwa Covid-19, ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona hawaonyeshi dalili za ugonjwa huo.

CNN juzi ilikaririwa ikiripoti kuwa, makadirio ya maambukizi ya ugonjwa huo yalipanda kutoka asilimia 30 mwishoni mwa mwezi Mei, mwaka huu, wakati CDC ilikadiria kwamba uwezekano wa kusambaa kutoka watu ambao hawaoneshi dalili ni asilimia 75.

Wakati maeneo kadhaa kusini na magharibi kwa Marekani walisajili maongezeko ya dhahiri ya visa na watu kulazwa kutokana na covid-19, taasisi kubwa ikiwemo CDC na Shirika la Afya Duniani (WHO) wametoa taarifa mpya kuhusiana na kusambaa ugonjwa huo unaosababishwa na Virusi vya Corona, Business Insider iliripoti juzi.

Sasa muongozo mpya wa CDC unakadiria kuwa asilimia 40 ya watu walioambukizwa Covid-19 hawana dalili za ugonjwa huo, na kwamba uwezekano wa kusambaa kutoka kwa watu kundi hilo ni asilimia 75.

Kupitia muongozo huo ambao pia ulichapishwa na CCN, wakala hiyo iliongeza “makadirio yake ubora kwa sasa” kwa kuwianisha na takwimu za mwishoni mwa mwezi uliopita na kuongeza wastani wa idadi ya watu walioambukizwa covid-19 ambao hawana dalili za ugonjwa huo kutoka asilimia 35 , ambayo iliripotiwa mwishoni mwa Mei, kufikisha asilimia 40.

Wakala hiyo awali walikadiria kwamba uwezekano wa kusambaa virusi hivyo kutoka kwa watu wasio na dalili ilikuwa ni asilimia 100, CNN ilikaririwa.

Ripoti mpya hiyo pia inajumuisha takwimu za ‘Wastani wa vifo kwa maambukizi’ ambayo inalinganisha makadirio kati ya watu wanaofariki kwa Covid-19 wenye dalili na wasio nazo, na hata walioshambuliwa vikali na ugonjwa huo.

Kulingana na matokeo ya majaribio mapya, CDC wamekadiria kuwa asilimia 0.65 ya watu walioambukizwa Covid-19 inatabirika watafariki.

Julai 9, mwaka huu, WHO waliongeza tahadhari kuhusu ilivyo rahisi virusi hivyo kusambaa baada ya kutambua kwa mara ya kwanza kwamba, Kirusi cha Corona hicho kinaweza kusambaa hewani kupitia aerosols, ambazo huweza kuelea futi kadhaa, imeripotiwa.

Takwimu mpya hizo zilizorekebishwa kuendana na hali ilivyo kulingana na wakati, zimetoka baada ya mamia ya wanasayansi na wahandisi kuwaandikia barua WHO wakitaka wabadili mtazamo wao kuhusiana na maambukizi ya ugonjwa huo, ambao walishasema kuwa kirusi kinachoeneza kilisambaa kupitia vimiminika ambavyo ni vikubwa zaidi na vizito, na huanguka kutokea hewani kwa kasi kuliko aerosols.

Watu wasio na dalili za ugonjwa huo,ambao wanaambukiza, pia wanasababisha hofu kwa maofisa wanaopambana kwa kutumia mipango ya kudhibiti ugonjwa huo ili shule zifunguliwe.

Shule wilayani na watu wanaotembea barabarani kote Marekani wameelezea hofu zao kuhusu shule kufunguliwa wakati ikiwepo milipuko ya ugonjwa huo majimboni na miongozo mipana ya usalama inayoelekezwa na CDC, ingawa kuna shinikizo kutoka utawala wa Rais Donald Trump.

Ingawa watoto wametambuliwa kama kada ya wanajamii walio katika hatari kidogo zaidi ya kuugua vibaya na kupoteza maisha kutokana na covid-19, CDC wamesema kuwa wanaweza kuwa kama wasio na dalili na wanaoambukiza pia virusi vinavyosababisha ugonjwa huo vya corona, na kwamba wanaweza hata kusababisha maambukizi kwa watu walio katika hatari zaidi kuambukizika ugonjwa huo.

Daktari Mkuu Marekani, Jerome Adams alikaririwa Jumapili akisema kuwa ingawa kuna takwimu zilizosajiliwa kubwa zaidi siku zilizopita za mlipuko wa ugonjwa huo, Marekani inaweza ikageuza mwenendo wa kusambaa maambukizi ya virusi vya covid-19 katika muda wa wiki mbili hadi tatu iwapo “kila mtu atawajibika kivyake” kwa kuzingatia ushauri wa kudhibiti unaopendekezwa na wataalam wa afya.

“Hivyo kama tulivyoona visa vikiongezeka kwa kasi, tunaweza kugeuza huu mwenendo upinduke katika wiki mbili hadi tatu, kama tunaweza kushawishi watu wengi wakaidi wavae vifunikanyuso, kukaa umbali angalau futi sita, kufanya mambo ambayo tunajua yanawezesha ufanisi,” amesema.