October 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Magreth agawa Reja umoja wa wanawake Kipawa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

DIWANI wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Magreth Cheka, amegawa reja za Umoja Wanawake UWT kata ya Kipawa ,Katika ziara yake endelevu kutembelea kukagua uhai wa chama na Jumuiya ya Wanawake UWT.

Akigawa reja hizo kata ya Kipawa Diwani Magreth Cheka ,alisema wamegawa reja hizo kwa ajili ya kujua Takwimu za Wanawake wa UWT kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani mwaka 2025.

“Ziara yangu ya kawaida mimi Mlezi wa Umoja wanawake UWT ninatekekeza agizo la Mwenyekiti wa UWT Taifa Mery Chatanda kujua takwimu za Wanawake wa UWT ili tujipange na chaguzi zetu zilizo mbele za Serikali ya Mtaa na Uchaguzi mkuu mwaka 2025″alisema Magreth.

Diwani Magreth alisema mara baada kugawa reja hizo za Umoja wanawake UWT ziara itaanza nyumba kwa nyumba kuakikisha wanawake wote wanawafikia na kuwapa kadi za wanawake.

Aliwataka viongozi wa uwt kata Kipawa kila tawi kuakikisha wanaanza ziara ya nyumba kwa nyumba kuafikia makundi ya wanawake yote waweze kuwakiki na kuwajaza katika reja ya wanawake ili muda wa uchaguzi ukifika wakikishe chama cha Mapinduzi CCM kinashika dola katika chaguzi zake zote ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani.

Aidha katika upande Mwingine Diwani Magreth Cheka aliwataka wanawake wa UWT kujenga umoja na mshikamano kuwa wamoja na kuimarisha chama na jumuiya .