Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amezindua mashindano ya Umoja wa Shule za Sekondari UMISSETA Wilaya ya Ilala iliyoshirikisha wanafunzi wa Jimbo la Ilala ,Segerea na Jimbo la Ukonga kwa ajili ya kuunda Timu ya wilaya Ilala kwa ajili ya mashindano ya Kanda.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo , alizindua mashindano hayo katika viwanja vya Pugu Sekondari Jimbo la ukonga ambapo yaliwashirikisha Wakuu wa shule za Sekondari zote za wilayani Ilala na viongozi wa TAHOSA Ilala pamoja na timu kutoka majimbo matatu.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo alisema Michezo ni sera ya chama cha Mapinduzi CCM ambayo ujenga afya na mahusiano katika jamii.
“Leo tunazindua mashindano haya ya wilaya Ilala nawaomba vijana wangu mkafanye vizuri katika timu ya Kanda muwe na maadili mazuri kambini na nidhamu bora muweze kuleta ushindi katika wilaya yenu kwa kuchukua vikombe vyote “alisema Mpogolo
Mpogolo alisema ofisi ya Mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na Meya wa Halmashauri ya jiji na Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam watakuwa karibu na Kambi ya Wachezaji wa Ilala mpaka watakapoenda andaa timu ya Taifa amewataka Wachezaji asilimia 90 watoke Ilala.
Alisema Michezo ni ajira na Wachezaji wa vipaji watakaotoka Ilala watakuwa nao karibu ili waweze kufika katika mashindano makubwa ikiwemo Ligi.
Alitumia fursa hiyo kupongeza Uongozi wa TAHOSA ,Mwalimu Mkuu wa Mwenyeji wa Shule ya Pugu Sekondari Juma Oreda na Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Mwalimu Mussa Ally kwa utendaji bora wa kazi na mahusiano mazuri katika idara ya Elimu Sekondari .
Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Ilala, Mwalimu Mussa Ally alisema jiji la Dar es Salaam Mwaka jana lilichukua vikombe 13 katika vikombe 17 ambapo mwaka huu Ilala imejipanga kuchukua vikombe vyote 17 natuma salam kwa wilaya Temeke,Ubungo,Kigamboni na Kinondoni waogope Wachezaji wa Ilala wapo vizuri kwa ushindi kutokana na maandalizi mazuri.
Diwani wa Kata ya Pugu Imelda Samjela alipongeza uongozi wa shule ya Sekondari Pugu na viongozi wa Umoja wa shule za Sekondari UMISSETA kwa maandalizi mazuri ya mashindano hayo ambapo aliwataka Wachezaji wa timu ya mkoa wa Ilala itakayoundwa wakafanye vizuri ili Ilala iweze kungara.
Alitumia fursa hiyo kuwataka Walimu wa shule za Sekondari hasa wa sekta za Michezo wachape kazi waendelee kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika sekta ya michezo kwani Michezo ya UMISSETA inaibua Wachezaji mbali mbali hadi wa timu za Taifa
More Stories
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship
Mnzava apania kuwapeleka vijana Simba na Yanga